Mlipuko wabomu umetokea leo nje ya mgahawa mmoja uliokuwa umejaa wateja wakipata chakula cha mchana huko Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo na kuuwa watu wasiopungua watano.
Mgahawa huo unaopatikana katika wilaya ya Hamarweyne, upo karibu na makao makuu ya manispaa ya serikali na katika eneo la kibiashara lenye shughuli nyingi.
Mohammed Mahdi ambaye ni mmoja wa watu walioshuhudia mlipuko huo amesema kuwa aliwaona watu wasiopungua watano wakiwa wametapakawa na damu nje ya makao makuu hiyo ya majengo ya manispaa ya serikali, huku shuhuda mwingine kwa jina la Yusuf Ali akisema kuwa mlipuko huo wa bomu la kutegwa garini ulitokea wakati eneo hilo likiwa limejaa watu wengi wakifanya manunuzi.
Kundi la kigaidi la al Shabab lenye uhusiano na mtandao wa al Qaida limekuwa likitekeleza mashambulizi makubwa dhidi ya maafisa wa serikali ya Somalia na vikosi vya kulinda amani vya kimataifa na vilevile kuzishambulia hoteli na migahawa huko Mogadishu. Nchi jirani ya Kenya pia ambayo imetuma wanajeshi wake kupambana na al Shabab huko Somalia imekumbwa na mashambulizi kadhaa kutoka kwa kundi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: