Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
1:52 PM
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akimuangalia mmoja
wadume la ng’ombe anayetumika kuzalisha Mitamba kwenye kitaru namba 9
shamba la kitengule-Karagwe.
Baadhi
ya ng’ombe waliopo kitaru namba 9 shamba la kitengule ambapo
kwenye block hii moja kuna Ng’ombe zaidi ya 800 wanaolishwa na
kuhudumiwa vizuri na mmiliki wa kitaru hiki
.Ng’ombe
wakitoka kuogeshwa kwaajili ya kuua baadhi ya wadudu kama
kupe wanaopendelea kukaa kwenye mwili wa ng’ombe.Hili ni moja ya josho
la kisasa ndani ya kitaru namba 9.
Kufuatia
ziara ya waziri mkuu,Mh:Kassim Majaliwa ndani ya mkoa wa Kagera
akiwa ameambatana na waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu
Waziri wa Mambo ya ndani,Ziara hiyo imekuja na maagizo kadhaa ikiwamo
wamiliki wote wa vitaru kwenye ranchi za Taifa ambao hawajaziendeleza
waziachie mara moja na maeneo hayo yagawiwe upya,Waziri Mkuu ameagiza
pia kwa wamiliki wa vitaaru ambao sio watanzania wajisalimishe au
waondoke kwenye vitaru hivyo kabla hatua kali hazijaanza kuchukuliwa.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na timu yake
ya wataalamu wameshaanza kupitia vitaru vyote “blocks” na wamiliki
wake ikiwepo pia idadinya mifugo kwa kila block,Hii leo Mwigulu
Nchemba amekutana na wamiliki wa vitaru kwenye shamba la
Kitangile-Karagwe na kuagiza wamiliki wote ambao hawajaendeleza maeneo
wanayoyamiliki yanachukuliwa na serikali kwaajili ya kuwapatia
watanzania wenye uwezo wa kuziendesha.
Mwigulu
Nchemba ameagiza pia wamiliki wa vitaru kuacha mchezo wa kukodisha
na kuingiza mifugo kutoka kwa wafugaji haramu wa nchi jirani,kitendo
hicho ni kosa na yeyote atakayebainika anakwenda jela na adhabu kali
itafuta. Mbali na vitaru hivyo,Waziri Mkuu akishirikiana na waziri wa kilimo wameagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera kuondoa wavamizi wote kwenye pori tengefu ya serikali kabla hatua zingine zinazofuata kuanza kutekelezwa.
Kupitia
uwekezaji mzuri kwenye kitaru namba 9 cha shamba la
Kitengule,Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa wafugaji wote nchini kuanza
kujipanga kufuga kwa mfumo wa vitaru ili kuachana na ufugaji holela
unaopelekea migogoro mbalimbali na wakulima.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: