MJI WA TRIPOLI WAGEUKA UWANJA WA MAPIGANO YA MAKUNDI HASIMU

Mji wa Tripoli wageuka uwanja wa mapigano ya makundi hasimu
Mji mkuu wa Libya, Tripoli jana uligeuka na kuwa uwanja wa mashambulizi makali ya silaha na hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wakazi wake.
Mapigano hayo yaliibuka baada ya makundi mawili ya wabeba silaha, kushambuliana vikali kwa silaha za kivita mjini hapo. Hata hivyo hadi sasa haijafahamika chanzo halisi cha kuibuka mapigano hayo yaliyoshuhudiwa katika maeneo ya Zawiyat al-Dahmani na Babu Aziziyyah, kama ambavyo pia majina ya makundi yaliyohusika katika mapigano hayo bado hayajafahamika. Itafahamika kuwa, makundi kadhaa nchini libya yanasimamia sheria katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu huo wa Libya, Tripoli, suala ambalo kwa mara kadhaa limekuwa likisababisha msuguano kati ya makundi hayo. Wakati hali ikiwa hivyo, kundi la Answaru Sharia, na kundi la kigaidi la Daesh, yameendelea kujizatiti nchini humo kutokana na kuendelea migogoro ya kisiasa baina ya wanasiasa wanaowania nyadhifa za juu serikalini. Kwa mujibu wa weledi wa mambo, wanachama wengi wa magenge ya kitakfiri wameelekea nchini Libya kutoka Syria, baada ya kuzidiwa nguvu

0 comments: