MISS Tanzania, Lilian Kamazima, akitoka kwenye mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2016. Uzinduzi rasmi wa msimu wa mashindano makubwa kabisa ya urembo hapa nchini, Miss Tanzania 2016, yatazinduliwa Jumamosi Machi 19, 2016 kwenye hoteli ya Ramada iliyoko Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, amewaambia waandishi wa habari
 Miss Tanzania, Lilian Kamazima, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
 Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Hashim Lundenga, akiwa na Miss Tanzania Lilian Kamazima, wakati akiongea na waandishi wa habari Machi 17, 2016


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MSIMU mpya wa amshindano ya ulimbwende, yaani (urembo), ya Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2016, utazinduliwa rasmi Jumamosi Machi 19, 2016 kwenye Hoteli ya Ramada Resort iliyoko Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo nchini wakiwemo wabunifu wa mabvazi, mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini watakwepo.
Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Lino International, ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo Machi 17, 2016, alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.
Burudani zitakuwepo kama kawaida kunogesha tukio hilo la aina yake ambapo wasanii kama vile Lina na Wanne Star watakuwepo.
Lundenga ambaye alifuatana na Miss Tanzania wa sasa, Lilian Kamazima, na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania, alsiema, mara tu baada ya uzinduzi huo, tukio linguine kama hilo litafanyika jijini Arusha.
Pia mawakala watapatiwa semina ambayo itapangwa baada ya tukio hilo na kasha mashindano ya urembo kwa ngazi za vituo, wilaya, mikoa na kanda yatafanyika.
Makampuni kadhaa yamejitokeza kudhamini mashindano hayo ambapo Lundenga ameyataja kuwa ni pamoja na Ramada Resorts Dar es Salaam, Naf Beach Hotel Mtwara, Kitwe General Trader, CXC Africa, Mwandago Investment Limited, Break Point na GSM Media

 Lilian akitaniana na mmiliki wa blog ya Father Kidevu, Mroki Mroki
Lundenga(katikati), Lilian, (kushoto) na Bosco Majaliwa, Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania

0 comments: