LIBERIAYAFUNGA MIPAKA YAKE NA GUINEA CONAKRY BAADA YA WATU KADHAA KUFA KWA HOMA YA EBOLA KATIKA NCHI HIYO JIRANI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:24 AM
Serikali ya Liberia imechukua uamuzi wa kufunga mipaka yake na
Guinea Conakry baada ya watu kadhaa kufariki dunia katika nchi hiyo
jirani kwa homa ya Ebola.
Liberia imetangaza kuwa, sanjari na kuchukua hatua za kiafya kwa
ajili ya kukabiliana na kesi mpya za maambukizi ya Ebola, imechukua
uamuzi wa kufunga mipaka yake na jirani yake Guinea Konacry.
Liberia iumechukua uamuzi huo masaa kadhaa tu baada ya kuripotiwa
mripuko mpya wa homa hatari ya Ebola nchini Guinea Conakry ambao tayari
umesababisha vifo vya watu watano huku mamia ya wengine wakiaminika kuwa
wameambukizwa ugonjwa huo.
Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema kuwa, mripuko huo mpya umetokea katika kijiji cha Porokpara, kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Kesi mpya mbili za Ebola zilithibitishwa Ijumaa iliyopita Kusini mwa
mkoa wa Nzérékoré nchini Guinea Conakry. Kesi mpya zilithibitishwa siku
ambayo Shirika la Afya Duniani WHO lilitangaza kumalizika kwa mripuko wa
ugonjwa huo katika nchi jirani ya Sierra Leone.
Ebola imeua zaidi ya watu 11,300 tangu mwezi Desemba 2013 katika
mripuko mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa wa ugonjwa huo uliozikumba zaidi
nchi tatu za magharibi mwa Afrika za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Homa hiyo ya Ebola mbali na kusababisha vifo vya watu katika nchi hizo tatu, ilitoa pigo kubwa pia kwa uchumi wa nchi hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: