Licha ya kuripotiwa habari za kuhamishiwa serikali ya umoja wa
kitaifa ya Libya katika mji mkuu wa Libya Tripoli katika kipindi cha
chini ya wiki moja, Waziri Mkuu wa serikali iliyojitangazia yenyewe
mamlaka huko Tripoli, ametangaza hali ya hatari ya usalama katika nchi
hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Khalifa al-Ghwell, Waziri Mkuu wa serikali iliyojitangazia yenyewe
mamlaka, jana alitoa taarifa na kutangaza hali ya hatari ya usalama
katika nchi hiyo na akavitaka vikosi vya usalama viimarishe doria katika
maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo. Hivi karibuni, Martin Kobler, mjumbe
maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya alisema kuwa,
serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya itaundwa katika kipindi cha chini
ya wiki moja na kuhamishwa katika mji mkuu Tripoli. Tangazo hilo la
Martin Kobler liliungwa mkono na nchi jirani na Libya na hata madola
makubwa ulimwenguni. Baada ya tangazo hilo ilitarajiwa kwamba, joto la
mgogoro wa kisiasa wa Libya lingepungua na hivyo kushuhudia kufikia
tamati kipindi cha utawala wa serikali mbili ambao umekuweko nchini humo
tangu Agosti mwaka 2014. Utawala wa serikali mbili nchini Libya mbali
na kusababisha kutoundwa serikali ya umoja wa kitaifa umepelekea
kushadidisha kiwango cha ukosefu wa usalama na amani katika nchi hiyo.
Magaidi wa Daesh wanadhibuti maeneo mbalimbali ya Libya ukuwemo mji
wa Sirte mahala alipozaliwa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Kanali
Muammar Gaddafi. Harakati za kundi la Daesh huko Libya zimekuwa na
taathira hasi pia kwa usalama wa nchi jirani hususan Tunisia. Fauka ya
hayo, mgogoro wa wahajiri haramu na magendo ya binadamu nchini Libya ni
mambo ambayo nayo yameshtadi, kiasi kwamba, Jean-Yves Le Drian, Waziri
wa Ulinzi wa Ufaransa amesema kuwa, harakati za kundi la kigaidi la
Daesh, wimbi la wahajiri haramu na magendo ya binadamu ni mambo matatu
makuu hatari yanayoikabili Libya. Hapana shaka kuwa, mambo hayo yatakuwa
na matokeo mabaya pia kwa usalama wa Ulaya.
Filihali, Khalifa al-Ghwell Waziri Mkuu wa serikali ya Libya yenye
makao yake Tripoli amepuuzilia mbali vitisho na kuhatarishwa usalama wa
raia na wa ardhi ya nchi hjiyo na kutangaza kwamba, hakubaliaini na
suala la kuachia madaraka na kukabidhi hatamu za uongozi kwa serikali ya
umoja wa kitaifa.
Mwanasasa huyo amekwenda mbali zaidi na kutangaza kuwa, endapo
wajumbue wa serikali ya umoja wa kitaifa wataelekea Tripoli kwa ajili ya
kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa basi atawatia mbaroni na kuwatupa
korojkoroni.
kwa upande wake Faiz al-Siraj, Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya
ametangaza kuwa, serikali ya maafikiano ya kitaifa inatarajiwa kuanza
kazi zake huko Tripoli karibuni hivi.
Inaonekana kuwa, katika mazingira ya sasa Libya inakabiliwa na
mgogoro wa hisa na nyadhifa katika serikali ijayo ya maafikiano ya
kitaifa. Kuna baadhi ya mirengo nchini Libya ambayo inaona kuwa, maslahi
yao yatakuwa hatarini endapo kutaundwa serikali ya maafikiano ya
kitaifa katika nchi hiyo. Vikosi vya serikali ya Libya yenye makao yake
mjini Tripoli ambavyo vikiwa chini ya mwavuli wa muungano wa makundi
yenye kubeba silaha unaojulikana kama "Fajr Libi" kwa zaidi ya mwaka
mmoja na nusu sasa vimekuwa vikidhibiti akthari ya maeneo ya magharibi
mwa nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Tripoli vinaona kuwa, vyenyewe vitapata
hasara kwa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa uongozi wa Faiz
al-Siraj.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: