WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA UNHCR, JOYCE MENDS-COLE
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:37 AM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (watatu kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake,
Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba
Yahya (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke
(wapili kulia) wakielekea katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara hiyo
kwa ajili ya kumuaga Mwakilishi wa UNHCR nchini, iliyofanyika katika
Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini,
anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba
yake fupi, Waziri Kitwanga alimshukuru Mwakilishi huyo kwa ushirikiano
wake mzuri kati ya Wizara na UNHCR, pia alimtakia safari njema na
mafanikio mema arudipo nyumbani kwake. Joyce anatarajia kustaafu rasmi
katika nafasi hiyo mwezi ujao. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara
hiyo, Injinia Hamad Masauni, kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu, Meja
Jenerali Projest Rwegasira, na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini,
anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kumbukumbu yake
kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la UNHCR na Wizara.
Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake,
Joyce Mends-Cole akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (wapili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara hiyo, kwa
ushirikiano mkubwa waliompa wakati anaiongoza UNHCR. Pia katika hotuba
yake, Joyce alimpongeza Rais John Magufuli kwa uongozi wake mzuri pamoja
na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka katika Serikali yake. Wakwanza
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak
Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Simba Yahya, na Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
Wakimbizi, Harrsion Mseke.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrsion Mseke akizungumza katika
hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole
(watatu kulia). Katika hotuba yake, Mseke alimshukuru Joyce kwa
ushirikiano wake mkubwa aliouonyesha wakati wa uongozi wake. Wapili
kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye
aliiongoza hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar
es Salaam. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad
Masauni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest
Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akimuaga Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza
muda wake, Joyce Mends-Cole mara baada ya kumaliza sherehe fupi
iliyoandaliwa na Wizara ya kumuaga kiongozi huyo wa UNHCR. Hafla hiyo
fupi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo na
kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Wizara akiwemo Waziri wa Wizara hiyo,
Charles Kitwanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (wanane kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia
Hamad Masauni (watano kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Projest Rwegasira (wasaba kushoto), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi (wanne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wanne kushoto), Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini,
anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wasita kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara pamoja wa UNHCR mara baada ya hafla
fupi ya kumuaga Joyce, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Dar es
Salaam leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: