SAKATA LA ESCROW ASKOFU KILAINI NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA


Baba Askofu Methodius KilainiDar es Salaam. Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii. 
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow. 
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni). 
Akizungumza kwa simu jana, Askofu Kilaini alisema Rugemalira hupendelea kuchangia kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye peke yake aliyempatia mchango, bali kuna watu wengine wengi ambao wameshampatia na kazi yake ni kuipokea na kuifikisha sehemu husika. 
Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake, simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena. 
Hata hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na Gazeti la Mawio toleo la jana akisema fedha alizozipokea kutoka kwa Rugemalira ni kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kanisa Katoliki. 
“Ndiyo nimepokea fedha kutoka kwa James na hii siyo mara ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya kijamii,” alisema Askofu Kilaini. 

Alipotakiwa na gazeti hilo kuwataja wengine waliochangia kanisa lake na kama nao wamechanga kutoka kwenye fedha za akaunti ya escrow, alisema yeye hayumo kwenye michango hiyo.

0 comments: