Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
11:37 AM
Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati) akiwasihi Mbunge wa
Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy
wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.
(Picha na
Emmanuel Herman)Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali
(PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na
kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake
na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.
Juzi, kamati hiyo ya
Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo
amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba
ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma.
Kamati hiyo ilieleza
kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu
aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya
umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji.
Akiwasilisha
taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua
hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa
na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa.
Jana,
alieleza kuwa pendekezo la Kamati ya PAC kutaka mitambo ya IPTL
itaifishwe si sawa kwa kuwa kulingana na mkataba wa PPA kati ya Tanesco
na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha
(Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha mtambo huo ni kukiuka
makubaliano katika mkataba wa PPA wa Mei 26, 1995.
“Ukiukwaji wa
aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa
ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa.
Aidha, utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya
kufukuza wawekezaji.”
Gharama za uwekezaji
Kuhusu taarifa
ya kamati ya PAC kwamba mwaka 2004 Tanesco ilifungua shauri katika
Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Kiuwekezaji (ICSID 2)
kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya gharama za uwekezaji, Profesa Muhongo
alisema suala hilo si kweli.
Alifafanua kuwa Tanesco haijawahi
kufungua shauri lolote ICSID ya London au Mahakama yoyote dhidi ya Benki
ya Standard Charterd kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama
inavyoelezwa na PAC.
“Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa Oktoba 31,
2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai
malipo ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya
ushirika ya Malaysia kwa IPTL. Wahusika katika shauri hilo la ICSID 2 ni
SCBHK na Tanesco na wala siyo Tanesco na IPTL.”
Alisema
Februari 12, ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na shauri la SCBHK na Tanesco
na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata
hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na
pande hizo kutokuwa na mkataba wa kibiashara baina yao.
“Vilevile,
kupitia shauri la madai Na. 60/2014, lililofunguliwa na IPTL katika
Mahakama Kuu ya Tanzania Aprili 4, ilizuia utekelezaji wa maelekezo
hayo,” alisema.
Uwekezaji wa Sh50,000
Profesa Muhongo
alisema kuhusu madai ya PAC kuwa mtaji wa uwekezaji katika mtambo wa
IPTL ni Sh50,000 na kwamba huo ndiyo ungetumika kukokotoa gharama za
uwekezaji ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa, maelezo hayo siyo
sahihi.
Alisema ukweli ni kwamba kutokana na uamuzi ya ICSID 1
ya Julai 12, 2001, gharama za ujenzi wa mtambo wa Tegeta ni Dola za
Marekani 127.2 milioni kama ilivyoelezwa na taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Profesa Muhongo
alisema katika taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano
wa deni na mtaji utakuwa 70:30 ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za
Marekani 89.04 milioni na mtaji ni Dola za Marekani 38.16 milioni na
kwamba uamuzi huo haujabadilishwa na Mahakama yoyote au mtu yeyote.
“Tunakubaliana
kwamba fedha iliyopokewa kutoka mabenki ya ushirika ya Malaysia kama
mkopo ni Dola za Marekani 85.86 milioni ambazo kati ya Dola za Marekani
105 milioni zilizokuwa zimeidhinishwa,” alisema na kuongeza:
“Swali
la kujiuliza je, mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za
Marekani 85.86 milioni, huku gharama halisi ya ujenzi wa mtambo wa
Tegeta ikawa Dola za Marekani 127.2 milioni?
Alisema ni dhahiri
kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani 38.16 milioni ambazo
pia zimetumika kwenye uwekezaji na kwamba Kamati ya PAC haikuonyesha
fedha hizo kuwa sehemu ya uwekezaji.
PAP na umiliki wa hisa saba
Profesa
Muhongo alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za Brela za Desemba 31,
2013, uhamishaji wa hisa saba za Mechmar katika IPTL kwenda PAP
ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa asilimia 70
za IPTL. Alisema Kamati ya PAC imeeleza kuwa PAP siyo mmiliki halali wa
hisa saba za Mechmar katika IPTL lakini kamati imethibitisha kwamba
nyaraka za mauziano kati ya Mechmer na Piper Link zilipokewa na
Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP.
“Kwa uthibitisho huo, kamati inakubali kuwa hisa za Mechmer katika IPTL zinamilikiwa na PAP,” alisema Profesa Muhongo.
Akana kuwa dalali
Profesa
Muhongo alisema taarifa ya Kamati ya PAC kwamba yeye ndiye aliyekuwa
dalali mkuu aliyewakutanisha Harbinder Sethi na James Rugemalira siyo
sahihi kuwa tangu Novemba 9, 2011, Rita iliitisha mkutano na
kuwakutanisha wadau wote wa IPTL wakati yeye alikuwa hajateuliwa kwenye
wadhifa huo.
“Mimi kama ni dalali, udalali wangu ni kupeleka
umeme vijijini. Mimi kama ni dalali udalali wangu ni kusaidia wachimbaji
wadogo wa madini na kupeleka Watanzania kusoma masters (shahada ya
pili) duniani kote.”
Serikali kutokuchukua tahadhari
Waziri
alisema Kamati ya PAC, imeeleza kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya
kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa
kwa fedha kutoka akaunti ya escrow kitu ambacho alidai si kweli.
Profesa
Muhongo alisema kinga iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na
imezingatia athari yoyote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na
kutolewa kwa fedha katika akaunti ya escrow.
“Kwa hiyo, siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ilivyodaiwa na PAC.”
Madai ya Sh321 bilioni
Profesa
Muhongo alisema hoja ya PAC kwamba imejiridhisha kuwa madai ya Tanesco
ya Sh321 bilioni yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya
kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na Tanesco na IPTL kukubaliana kiwango
sahihi cha Capacity Charge haina nguvu.
“Madai ya kwamba
Tanesco inaidai IPTL Sh321 bilioni msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa
IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Sh50,000 kwa wakati huo. Dhana hii
ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani 38.16 milioni ziliwekezwa
kwenye mradi wa Tegeta,” alisema.
Profesa Muhongo alisema
Bodi ya Tanesco imekana kuyatambua madai hayo ya Sh321 bilioni...
“Kimsingi hata vitabu vya hesabu vya Tanesco ambavyo vimekuwa
vikikaguliwa na CAG, havionyeshi kuwapo kwa deni hilo.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: