Add caption
SHIRIKA
la Kikundi cha Huduma Majumbani Mkoa wa Mbeya(KIHUMBE) kwa ufadhili wa Shirika
la kuhudumia watoto duniani(UNICEF) limezindua Mpango wa Marekebisho ya tabia
na mpango wa utoaji msaada wa sheria kwa watoto wanaokinzana na Sheria.
Uzinduzi
huo ulifanywa na Kamishna Msaidizi Haki za Mtoto na marekebisho ya Tabia
nchini, Rubikira Mushi, katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa JM Motel
iliyopo Forest ya zamani na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali ambao ni wadau
wa watoto wakiwemo Dawati la jinsia la Polisi, Ustawi wa Jamii, Watendaji wa
kata, Msajili wa Mahakama, Chama cha Wanasheria na muwakilishi wa Unicef.
Akizungumzia
Marekebisho ya tabia kwa watoto wanaokinzana na sheria na waliokatika hatari ya
kukinzana na sheria, Meneja wa KIHUMBE, Samwel Ptolemy, alisema kutakuwa na
faida kubwa baada ya kuanza kutekelezwa kwa mpango huo kwa ufadhili wa UNICEF.
Ptolemy
alisema mpango huo utafanikiwa endapo uwepo wa rasilimali watu wa kutekeleza
mpango na kutoa mrejesho, kuweka sehemu ambayo watoto watapata mafunzo na elimu
kwa kushirikiana na wadau, Ushirikiano baina ya Wadau na Serikali katika kutoa
huduma ndani ya jamii.
Aliongeza
kuwa faida za mpango huo ni kupunguza idadi ya makosa ya jinai yanayowakumba
watoto baada ya kupatiwa elimu, mtoto ataweza kuhudhuria shughuli za maendeleo,
kuhudhuria masomo na hatimaye kubadili tabia na kuwa mtoto mwema katika jamii.
Kwa
upande wake mwakilishi wa UNICEF katika uzinduzi huo, Mbelwa Gabagumbi,
alisema mfumo wa ulinzi na usalama wa mtoto ni wajibu wa Serikali na kila
mwananchi hivyo ni vema kuheshimu mkataba wa kimataifa ambao Tanzania iliridhia
wa haki za watoto wa mwaka 1989.
Alisema
Tanzania kuna changamoto kubwa ya kufikia malengo kutokana na Halmashauri
nyingi kutotenga fedha za kutosha kwa ajili ya maswala ya ulinzi na usalama wa
watoto hali inayokwamisha utekelezaji wa mipango mbali mbali inayowekwa na
serikali.
Aliongeza
kuwa utafiti uliofanywa unaonesha baadhi ya Halmashauri kutenga asilimia 0.002
katika bajeti zao kwa ajili ya siku ya mtoto wa afrika na sio Ulinzi na usalama
wa mtroto kama mpango uliozinduliwa unavyotaka.
Akizindua
rasmi mpango huo, Kamishna msaidizi Haki za mtoto na marekebisho ya tabia,
Rubikira Mushi, mbali na kuyapongeza mashirika ya Kihumbe na Unicef pia
aliwapongeza wadau wa watoto Mkoa wa Mbeya kwa kuwa na uelewa wa kuhusu
matatizo ya watoto.
Alisema
Mpango ulishazinduliwa kwa mara ya Kwanza Mkoani Dar Es Salaam na kufuatiwa na Mkoa
wa Mbeya na kuongeza kuwa Sababu zilizopelekea Mkoa wa Mbeya kuwa pili
kuzinduliwa kwa mpango huo kuwa ni pamoja na uwepo wa dawati la jinsia la
Polisi.
Alizitaja
sababu zingine kuwa ni Uwepo wa ofisi za Waendesha mashtaka wa Serikali na
Wanasheria wa Serikali,Maafisa ustawi wa jamii wanaoshughulikia mashauri ya
watoto, Maafisa ustawi wa jamii hadi ngazi ya kata, timu imara ya ulinzi na
usalama wa watoto pamoja na Chama cha Tanganyika Law Society(TLC) kujitolea
kutoa msaada bure kuhusiana na maswala ya watoto.
Aliongeza
kuwa sababu nyingine ni kuonekana kwa watoto wadogo katika magereza ya wakubwa
wakishikiliwa kwa makosa mbali mbali jambo lililopelekea kuzinduliwa kwa mpango
huo katika Mkoa wa Mbeya.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
0 comments: