Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:39 AM
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kufuatia
vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili iliyopita baada ya
msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kucheleweshwa kupanda stejini
kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani,
mwanamuziki huyo anadaiwa kupigwa marufuku kutia maguu nchini humo.
Viti
vya ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani
vilivyoharibiwa na mashabiki waliopoteza uvumilivu kusubiri shoo ya
Diamond Platinum.
“Tukio la
vurugu za Diamond limeripotiwa kwenye magazeti tofauti mjini hapa lakini
kubwa ni hasira ambayo mashabiki wa Diamond wameionesha waziwazi.
“Kwa mfano Gazeti la Stuttgarter la leo (Jumatatu) la mjini hapa limeandika:
‘MASHABIKI WANA HASIRA NA DIAMOND’.
Kwenye habari zao waliwahoji watu waliofurika ukumbini hapo.
“Wengi walikuwa wakilalamika kwamba walikata tiketi mapema kwa euro
25 (zaidi ya Sh. elfu 55) kwa kichwa. Yaani kuanzia saa 4:00 watu
walikuwa tayari wanamsubiri Diamond.
MUDA WAYOYOMA
“Kuna muda DJ alitangaza kwamba angepanda stejini kuanzia saa 6:00
usiku hivyo watu wakapunguza hasira. Cha ajabu saa saba ilikatika, nane
ikapita, tisa ndipo mtiti ukaanza.
“Sasa
hebu fikiria mtu umetoa buku 55 yako halafu hadi saa tisa usiku mtu
haonekani! Hapo ndipo tatizo lilipoanzia!” yamesomeka hivyo magazeti ya
hapa.Ilisemekana kwamba ilipofika saa 10:00 alfajiri ndipo Diamond
alipoletwa jukwaani na promota wake, raia wa Nigeria anayejiita
Kamabritts.
CHUPA ZARUSHWA
Mashabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na
kutaka kumvamia mwanamuziki huyo na promota wake.Ilidaiwa kwamba
kilichowakera zaidi mashabiki hao ni vyombo vibovu vilivyofungwa
ukumbini humo kitu ambacho kiliwafanya kuvunjavunja viti, meza, jukwaa
na vyombo vya muziki kisha kusababisha watu kujeruhiwa na hasara kubwa
ya mamilioni ya shilingi.
MAJERUHI WAONGEZEKA
Baadhi ya vyombo vya habari mjini humo, juzi (Jumatatu) viliripoti
kuongezeka kwa majeruhi wakiwemo MaDJ wawili ambao hali zao bado ni tete
hospitalini kwa sasa.
Katika vurugu hizo, DJ mwanamke aliyetajwa kwa jina la DJ Flor
alizimia hivyo akakimbizwa hospitalini huku mashabiki wakimpa kipigo DJ
Drazee.
KAULI YA POLISI
Polisi eneo la Sindelfingen, Stuttgart nchini Ujerumani walisema
tukio hilo ni la aibu hivyo uchunguzi wa kina unaendelea ambapo promota
huyo na Diamond watalazimika kulipa vitu hivyo na kwamba hawatawaruhusu
kufanya tena shoo eneo hilo na kwingineko nchini humo.
Vyombo
vya habari vya Ujerumani viliandika kuwa polisi wamesema walitenga
askari 18 wa kutuliza ghasia ambapo walifyatua mabomu ya machozi ili
kumuokoa Diamond.Walisema kwamba kitendo cha msanii kuchelewa kufika
jukwaani nchini humo ni kitu cha hatari mno kwani mashabiki wanaheshimu
muda wao.
PROMOTA ASAKWA
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni polisi walikuwa wakimsaka
promota huyo, Kamabritts ili wamalizane na Diamond aruhusiwe kuondoka
nchini humo na asirudie tena jambo kama hilo.
MCHEZO NYUMA YA PAZIA
Duru za kiuchunguzi zinaonesha kwamba, shoo nyingi za wasanii kutoka
Afrika zinazofanywa kwenye kumbi mbalimbali katika baadhi ya nchi za
Ulaya, hucheleweshwa makusudi ili vinywaji viuzike.
'Mzee wa Mdogomdogo', Diamond Platinum taratiiiibu akiondoka eneo la tukio huku gari likishambuliwa na washabiki wenye gadhabu.
Ilidaiwa
kwamba, katika tukio hilo baya, kulikuwa na tatizo la kiusimamizi kwani
mbali na promota, menejimenti ya Diamond ilipaswa kuwa na ratiba kamili
na siyo kumsikiliza promota ambaye anawaza zaidi kuingiza kipato kuliko
heshima ya msanii hivyo jamaa huyo kuwa staa wa kwanza kutoka Afrika
Mashariki kusababisha vurugu Ulaya.
LAWAMA KWA MENEJA WA UJERUMANI
Kuna maelezo kwamba, Diamond huwa ana mameneja wengi kwenye kila nchi
anayokwenda hivyo huyo meneja wa Ujerumani alistahili lawama zote kwani
alipaswa kujua kinachoendelea ukumbini.
BABU TALE ANASEMAJE?
Kuhusu hilo, Risasi Jumatano lilimtafuta meneja wa Diamond ambaye
hakusafiri na msanii huyo, Babu Tale na kuulizwa kulikoni yaliyomkuta
Diamond Ujerumani ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kweli inasikitisha lakini haukuwa mpango wa Diamond. Ninachojua alikuwa akimsikiliza promota.
Ni
changamoto kubwa lakini tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wa Ujerumani.
Next time wampokee vizuri.“Lakini kwa upande mwingine unajua ni jambo
kubwa na niseme tu kuwa ukilitazama tukio hili kibiashara ni kama
limemkuza zaidi kujulikana duniani. Umeona ameripotiwa na vyombo vingi
vya habari. Mitandao ya kijamii ndiyo usiseme. Yote kwa yote tumejifunza
na tunaomba radhi. Tusiangalie tulipoangukia, tuangalie tulipojikwaa.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: