ZITTO Kabwe aombwa kuwa mgeni rasmi katika jubileni ya miaka 25 ya Pomerini Sekondari


Mkuu wa shule ya Sekondari Pomerin Bw Shadrack Nyaulingo
Wanafunzi wa kidato cha nne Pomerini wakijisomea
Mwalim wa taalum shuleni hapo
Mwanafunzi wa Pomerin wakijis
omea
Baadhi ya mabweni ya shule hiyo
wanafunzi wakijiandaa kwenda katika michezo
Na Matukiodaima.co.tz
MWENYEKITI wa kamati ya bunge hesabu za serikali (PAC) Zitto Kabwe ameombwa kuwa mgeni rasmi katika jubilie ya miaka 25 ya shule ya sekondari Pomerin wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akizungumza leo na wanahabari mjini Iringa mkuu wa shule hiyo Shadrack Nyaulingo alisema kuwa wamemwandikia barua ya kumwomba Kabwe kuja kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za shule kutimiza miaka 25 toka ilipoanzishwa na kuwa mbali ya kuazimisha miaka hiyo 25 pia wataendesha harambee kwa ajili ya uboreshaji wa majengo ya shule hiyo ambayo kwa sehemu kubwa yapo katika hali mbaya zaidi.

" Tumemwandikia barua ya kumwomba mheshimiwa Zitto kuja kuwa mgeni rasmi kutoka na kingozi huyo kuwa ni mmoja kati ya wadau wa maendeleo katika mkoa wa Iringa hasa ukizingatia kuwa alisoma katika shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo mkoani Iringa..... hivyo tumeona tumwombe kuja kusaidia kuendesha harambee kama sehemu ya kutambua mchango wake katika Taifa "

Nyaulingo alisema kuwa jumla ya kiasi cha Tsh milioni 61 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo na kuwa mbali ya kumwandikia barua Kabwe ambae ni mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazin bado wamesambaza barua kwa watu mbali mbali wakiwemo wabunge wa CCM kama mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe, mbunge wa jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla, mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati pamoja na makada na watu mbali mbali kama Salim Asas, Frederick Mwakalebela na wengine

Alisema kuwa pia wanafunzi mbali mbali ambao wamesoma katika shule hiyo wamealikwa na kuombwa kuchangia ukarabati wa shule hiyo huku akiwataka wale wote watakaohitaji kusaidia ukarabati wa shule hiyo kutuma mchango wao kupitia akaunti ya NBC 028103002306 na CRDB ni 01J2070000100 ama M-pesa kwa namba 0768911120

Mkuu huyo alisema shule hiyo ambayo ilijengwa miaka 50 iliyopita na wajerumani ilikuwa ikitumika kama shule ya msingi kabla ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa kuichukua na kuifanya sekondari miaka kwa miaka 25 sasa .

Hata hivyo alisema kuwa mbali ya kanisa kufanya ukarabati mkubwa ila bado baadhi ya majengo yana hali mbaya kiasi cha kuhitaji kufanyiwa ukarabati zaidi hasa na paa kutokana na sehemu kubwa ya majengo paa zake kuwa katika hali ya uchakavu mkubwa .

Akielezea kuhusu ubora wa elimu shuleni hapo alisema kuwa kati ya shule bora katika mkoa wa Iringa na Tanzania ni pamoja na Pamoreni kutokana na rekodi nzuri iliyopo kwa kuendelea kushika nafasi ya shule 20 bora katika matokeo ya kidato cha sita na shule ya pili kimkoa kwa kufanya vema katika matokeo hayo ya kidato cha sita .

Alisema kuwa jubilei hiyo ya miaka 25 ya shule hiyo itafanyika Octoba 25 mwaka huu na hivyo kuwaomba wanafunzi wote waliosoma katika shule hiyo na wafanyakazi waliopata kufanya kazi kushiriki katika sherehe hizo ili kujumuika na mgeni rasmi na wadau wa maendeleo mkoani hapa katika harambee hiyo.

0 comments: