Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
12:06 PM
MONROVIA,
LIBERIA WANAUME waliokuwa na silaha waliodai kwamba hakuna maradhi ya
Ebola Liberia, walivamia eneo ambalo wanaougua ugonjwa huo walikuwa
wametengwa jijini Monrovia.
Walioshuhudia
kisa hicho kilichotokea Jumapili walisema wakati wa uvamizi huo,
wagonjwa 20 walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo walitoroka. “Walivunja
mlango na kupora mali eneo hilo.
Wagonjwa
wote wametoroka,” alisema Bi Rebecca Wesseh, aliyeshuhudia uvamizi huo.
Mkuu wa chama cha wahudumu wa afya wa Liberia, Bw George Williams na
wakazi wa jiji hilo walithibitisha ripoti hizo.
Williams
alisema eneo hilo lilikuwa na wagonjwa 29 waliokuwa wakichunguzwa kabla
ya kupelekwa hospitali. Hata hivyo, haikubainika idadi ya wagonjwa ambao
hawakujulikani waliko.
“Wote
walipatikana kuwa na Ebola,” alisema na kuongeza bila kufafanua kuwa
tisa walikufa. Bi Wesseh alisema alisikia wavamizi hao wakipiga kelele
wakisema Rais Ellen Johnson Sirleaf “ hana pesa,” na kuongeza “
anatafuta pesa. Hakuna Ebola Liberia.”
Wesseh
alisema wavamizi hao ambao wengi waliokuwa vijana waliobeba rungu
walivunja mlango wa eneo lililotengwa kwa wagonjwa katika shule moja ya
pili viungani mwa Monrovia.
Alisema
wauguzi pia walitoroka wakati wa uvamizi huo. Vifo 1,145 Mkurupuko wa
Ebola wa sasa ndio mbaya zaidi tangu ugonjwa huo ugunduliwa kwa mara ya
kwanza 1976, na umeua watu 1,145, kulingana na takwimu za Shirika la
Afya ulimwenguni (WHO) zilizotolewa Agosti 13, 2014. Vifo 413 vimetokea
Liberia, 380 Guinea, 348 Sierra Leone na 4 Nigeria. Add a comment maoni
Source: Swahili Hub
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: