Majeshi 480 wa Nigeria watorokea Cameroon
Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.
Mapigano hayo yanawadia saa chache tu baada ya wapiganaji hao wa Boko Haram kutoa kanda ya video ambayo walitangaza kuundwa kwa himaya ya Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema
0 comments: