Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
12:34 PM
Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi akisoma Tamko hilo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa wanasikiliza kwa makini Tamko hilo
Waandishi wa Habari wakiendelea na kazi
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mbeya kimeisimamisha
kamati ya siasa Wilaya ya Ileje kwa utovu wa nidhamu pamoja na
kuwasimamisha viongozi wa Chama hicho kata ya Majengo wilaya ya Momba
mkoani Mbeya.
Hayo
yalibainishwa jana na Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya,
Bashiru Madodi, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisi za CCM
Mkoa wa Mbeya zilizopo Sokomatola jijini Mbeya.
Madodi
alisema maamuzi hayo yalifikiwa Agosti 23, mwaka huu baada ya kamati ya
siasa ya Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Godfrey Zambi kufanya zxiara ya
ghafla katika maeneo hayo.
Madodi
alisema katika Wilaya ya Ileje chanzo kikubwa cha hali hiyo kutokuwepo
kwa maelewano baina ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Katibu wake hali
iliyopelekea kufunga ofisi kwa muda wa siku kumi.
Alisema
kutokana na kuwepo kwa mtafaruku huo Kamati iliamua Kuvunja kamati ya
Siasa ya Wilaya ya Ileje, ilipendekeza Vikao vya juu kwa maana kamati
kuu ya CCM Taifa imvuee Uenyekiti Hezron Kibona.
Alisema
Kamati pia imeagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje
Mohamed Mwala na katibu wa Baraza la Madiwani wa CCM kupewa onyo kali na
kuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 12 na kutoruhusiwa kuhudhuria
vikao vya kamati ya siasa vinavyotokana na nyadhifa zao.
Pia
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ileje avuliwe madaraka na wajumbe wote
wa kuchaguliwa wa Kamati ya siasa Wilaya waondolewe moja kwa moja kuwa
wajumbe wa kamati ya sioasa ya Wilaya.
Madodi
aliongeza kuwa Kamati imemuagiza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa,
Janeth Mbene ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kufika
katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa ili kuhojiwa kutokana na kuwa
chanzo cha hali hiyo.
Madodi
alisema Kamati Pia ilikutana na Kamati aya Siasa ya Momba na kukuta
mgogoro wakiwatuhumu viongozi wao kutumia vibaya mali ya chama ambayo ni
mapato ya kodi ya Majengo.
Aliwataja
viongozi hao Mwenyekiti wa Kata ya Majengo Ndugu Daniel, Katibu wa
Kata, Hemed Steven na Katibu wa Fedha na uchumi ambapo pia kamati
imeundwa ili kufuatilia hali halisi iliyofujwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: