TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02.07.2014.
• MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA USONI NA MTOTO WAKE.
• WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO]
•
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI
WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MARTHA KYANDO (73) MKAZI WA KIJIJI CHA
IBUNGILA AMEUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA USONI KISHA KUNYONGWA
SHINGO NA MTOTO WAKE AITWAE KISWIGO ANGANISYE (33) MKAZI WA KIJIJI CHA
IBUNGILA WILAYANI RUNGWE.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 00:30 USIKU KATIKA
KITONGOJI CHA MPUNGUTI, KIJIJI CHA IBUNGILA, KATA YA MALINDO, TARAFA YA
UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. AIDHA INADAIWA KUWA KABLA YA
KUUAWA MAREHEMU PIA ALIBAKWA.
INADAIWA
KUWA CHANZO CHA TUKIO NI BAADA YA MTUHUMIWA AMBAYE INASEMEKANA ANA
MATATIZO YA AKILI KUCHUKIA BAADA YA MAREHEMU KUMPIKIA MAGIMBI BADALA YA
UGALI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KOSA LA
KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1.
EMANUEL SAKALA (21) MKAZI WA MWANJELWA, 2. SHABAN ZUBERI (23) MKAZI WA
MWANJELWA 3. JAMES ANDREW (24) MKAZI WA MAKUNGULU 4. MIKIDADI MWALUGOYA
(25) MKAZI WA MWANJELWA 5. SADIKI HUSSEIN (24) MKAZI WA JUAKALI.
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA WAKIWA NA GONGO UJAZO WA LITA 5 KATIKA MSAKO ULIOFANYWA
KATIKA ENEO LA BENKI – MWANJELWA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA,
JIJINI MBEYA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA.
WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA
NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WAHAMIAJI HAO
HARAMU NI PAMOJA NA 1. THOMAS JUMA (29) NA 2. BONIFACE CHITETE (29).
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 23:15 USIKU
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA KATIKA ENEO LA KYELA- KATI, KATA YA KYELA-KATI,
TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA
KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU
WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI
HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments: