BASI LA LUSHANGA LAUWA MMOJA NA KUJERUHI WAWILI SEGEREMA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:59 AM
Kijana
ambaye ni dereva wa toroli la miguu minne jina lake halikuweza
kupatikana mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32 amefariki
dunia papo hapo na kupasuka Kichwa baada ya kugongwa na basi la abiria
lililokuwa likitokea mkoa wa Geita kuelekea jijini Mwanza kwenye
makutano ya barabara ya Kamanga na Busisi wilayani Sengerema mkoani
Mwanza. Kijana huyo pia alikuwa akiendesha Pikipiki bila kuvaa “Helmet”
huenda ingemsaidia asipasuke Kichwa.(Picha na Zainul Mzige).
Na MOblog, Sengerema
Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina lake mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38
(mwanaume)
kufa papo hapo Na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari
kwenye makutano ya barabara ya Kamanga na Busisi wilayani Sengerema
mkoani Mwanza.
Tukio
hilo limetokea jana Juni 30 majira ya saa 9 alasiri ambapo basi la
abiria mali ya kampuni ya Lushanga lenye namba za usajili T 312 ATA
likiwa na Abiria likitokea Mkoa wa Geita kuleleka mkoani Mwanza kupitia
kivuko cha Kamanga.
Marehemu
alikuwa anaendesha troli lililokuwa limebeba miti ambapo amepasuka
kichwa na kusababisha Ubongo kutoka nje, na mwili wake umepelekwa katika
hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya uchunguzi zaidi
pamoja na majeruhi kwa ajili ya matibabu.
Baadhi
ya wakazi wa Sengerema wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kijana
mwingine aliyepasuka eneo la jichoni baada ya ajali hiyo kutokea. Kijana
huyo alionekana kuchanganyikiwa pamoja na maumivu makali baada ya
kutokea ajali hiyo.
Kwa
upande wa mashuhuda abiria waliokuwa katika basi hilo hakuna
aliyejeruhiwa katika ajali hiyo pamoja na gari hilo kuharibika baada ya
kushindwa kuendelea na safari hivyo kurudi nyuma na kujikita kwenye
mtaro.
Hadi
tunaandika habari hii chanzo cha ajali hii hakijajulikana kutokana na
uchunguzi wa polisi wilayani humo kuhusu ajali hiyo kuendelea na dereva
wa basi hilo na konda wake waliotokomea kusikojulikana kutokana na
mkusanyiko wa watu eneo la tukio.
Tutakuletea taarifa zaidi baada ya Polisi kutoa ripoti ya chanzo cha ajali hiyo.
Raia
wema wakijaribu kumtuliza mmoja wa majeruhi alale chini kwa muda
kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kuasuka eneo la karibu na jicho
lake huku mwendesha Baiskeli naye akiwa amepoteza fahamu kwa muda.
Mwendesha
Baiskeli akiwa amezinduka huku dereva wa Bodaboda akionekana kuwa na
maumivu makali kutokana na kuchanika eneo la jicho lake.
Baadhi
ya wakazi wa Sengerema wakiangalia basi la abiria lilisobabisha ajali
hiyo kutokana na mwendo mkali alipokuwa akikunja kona na kushindwa
kuzuia basi hilo na mwishowe kujikita kwenye mtaro. Wengine ni wakazi wa
Sengerema wakijaribu kuangalia chini ya uvungu wa gari kama kuna mtu
amefunikwa na basi hilo.
Umati wa wakazi wa Sengerema ukiwa umefurika eneo la tukio kushuhudia ajali hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Sengerema wakingalia maiti ya mwendesha Bodaboda aliyefariki papo hapo baada ya ajali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: