MADEREVA TAXI MKOANI NJOMBE WAGOMA, KISA USHURU MKUBWA
Wakizungumza
madereva na wamiliki hao wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Njombe wamesema kuwa wanashangazwa kuona wameanza
kukamatwa kwa kutolipia ada ya mwaka ili hali hawajarudishiwa majibu ya
makubaliano walioafikiana kwenye kikao cha mwaka 2011 kilichofanyika
katika ukumbi wa halmashauri hiyo kuhusiana na mapendekezo ya ada ya
magari hayo.
Aidha
wamiliki na Madereva hao pamoja na kulalamikia utaratibu uliowekwa na
halmashauri hiyo lakini wamekubaliana kusimamisha zoezi la kulipa ada
hadi viongozi wa halmashauri hiyo wakalijadili kwenye vikao vya ndani
huku baadhi ya madereva waliobadilisha stika kwenye magari yao
wakitakiwa kwenda kuyasajili upya.
Wakizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo maafisa biashara wa
halmashauri ya mji wa Njombe Petter Kalihose na Edward Mdem wamekubali
kusimamisha ada hiyo hadi suala hilo likajadiliwe kwenye vikao vya ndani
na mkurugnezi juu ya kuongezewa kwa muda wa kusajili magari mapya
yaliobadilishiwa stika za magari pamoja na Ada ya mwaka huku magari
ambayo hayakusajiliwa kabisa wakiendelea na zoezi la kuyakamata.
Diwani
wa kata ya Njombe Mjini Agry Mtambo akiwa kwenye mkusanyiko wa
madereva na wamiliki hao amewasihi kwenda kuyasajili magari
yalionunuliwa hivi karibuni na kuwekewa stika za gari lililouzwa huku
akisema halmashauri itaweka utaratibu mzuri wa kudai ushuru na ada za
magari na viongozi wa tax watajulishwa makubaliano ya kikao cha ndani
cha halmashauri hiyo.
Kwa
upande wao viongozi wa madereva na wamiliki wa tax Njombe mjini Akiwemo
katibu wao Richard Chyonya wamesema halmashauri inatakiwa
kuwashirikisha kabla haijachukua maamuzi kwani viongozi wapo wa tax wapo
kwa lengo la kuwasiliana na uongozi wa halmashauri ili kudai kodi na
ushuru mbalimbali na si kama utaratibu ulioanza kutumika.
Na Michael Ngilangwa
No comments:
Post a Comment