|
Rais
wa Baraza la habari Tanzania (MCT), Jaji mstaafu Dk. Robert Kisanga akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mwaka la Maadili ya Waandishi wa Habari
lililoenda sambamba na Mkutano Mkuu wa 17 wa Wanachama wa MCT, lililofanyika
katika eneo litakalokuwa Makao Makuu ya Baraza Kimalang’ombe wilayani Bagamoyo
mkoa wa Pwani Juni 24 – 25 mwaka huu. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi
Mukajanga, Makamu wa Rais wa MCT, Chande Omar (wa pili kushoto) na Katibu
Tawala wa Wilaya hiyo (DAS), John Mahali. PICHA ZOTE/JOHN BADI wa Daily
Mitikasi Blog |
|
Sehemu
ya wanahabari na wanachama wa MCT waliohudhuria kongamano hilo. |
|
Mwezeshaji
Rosemary Mwakitwange (kulia), akiendesha mjadala elekezi kuhusu changamoto za
mfumo huria wa habari, uzoefu wa vyombo vya habari kujisimamia: Kabla na sasana
changamoto za vyombo huria: Kuigawa
Nchi/Kuimarisha Demokrasia wakati wa kongamano hilo. Kutoka (kushoto) ni watoa
mada, Prof. Mlama, Ndimara Tegambwage na Jenerali Ulimwengu. |
|
Mwanachama
wa MCT, Simon Mkina akigawa karatasi za kupigia kura katikauchaguzi wa Rais,
Makamu wa Rais na Wajumbe wa Bodi ya MCT, wakati wa mkutano mkuu wa 17 wa
wanachama. |
|
Upigaji
wa Kura ukiendelea. |
|
Rais
wa MCT anayemaliza muda wake, Jaji Mstaafu Dk. Robert Kisanga akipanda mti
ndani ya eneo la yatakapokuwa makao makuu ya MCT mjini Bagamoyo. Kushoto ni
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga na (kulia), Makamu wa Rais wa MCT
anayemaliza muda wake, Chande Omar. |
XXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na John Badi
Daily Mitikasi Blog
Bagamoyo
MKUTANO Mkuu wa 17 wa Wanachama wa Baraza la Habari Tanzania
(MCT), umemchagua Jaji mstaafu Thomas Bashite Mihayo kuwa Rais mpya wa baraza
hilo, baada ya aliyekuwa Rais Jaji mstaafu Dk. Robert Kisanga kumaliza muda
wake.
Mkutano huo, ulioenda sambamba na Kongamano la Mwaka la
Maadili ya Waandishi wa habari ulifanyika katika eneo yatakapo kuwa makao makuu
ya baraza hilo, Kimalang’ombe wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani juni 24 na 25
mwaka huu.
Aidha katika uchaguzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji
Zanzibar (ZBC), Hassan Abdallah Mitawi alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa
Baraza hilo.
Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa kutoka kundi la jamii ni
pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa cha UDSM, Prof. Bernadetha
Killian, jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Juston Mlay na Mhandisi wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Mfanyabiashara maarufu Bw. Ali
Mufuruki.
Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa kutoka Tasnia ya Habari ni pamoja
na Rose Mwalimu Haji, Tuma Abdallah kutoka Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN),
Mkuu wa Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la The Guardian,
Warrace Maugo.
0 comments: