Matokeo ya awali ambayo BIN ZUBEIRY
imeyapata kutoka chumba cha kuhesabia kura ukumbi wa Bwalo la Maofisa
wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, Evans Elieza Aveva ameshinda Urais
kwa kupata kura 1452 kati ya 1845 zillizopigwa, mpinzani wake Andrew
Tupa akipata kura 387 wakati kura sita zimeharibika. Hata hivyo, matokeo
rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo
chini ya Mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro baadaye |
No comments:
Post a Comment