Mlipuko karibu na ubalozi wa Iran, mjini Beirut,
Lebanon
Watu wapatao 22 wameripotiwa kuuawa katika milipuko miwili
ambayo imepiga mfululizo karibu na ubalozi wa Iran katika mji mkuu wa Lebanon,
Beirut.
Afisa ubalozi wa Iran Ebrahim Ansari ni miongoni mwa waliouawa katika
milipuko hiyo. Maafisa wamesema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
Picha za televisheni zimeonyesha magari yakiungua, maiti zikiwa zimelala
mtaani na majengo yaliyoharibiwa.
Iran imekuwa ikikiunga mkono kikundi cha Hezbollah ambacho ni cha wapiganaji
wa madhehebu ya Kiislam ya Shia, ambacho kimetuma wapiganaji wake kwenda Syria
kusaidia serikali ya Rais Bashar al-Assad.
0 comments: