KINANA ATINGA PERAMIHO SONGEA NA KUWAKEMEA VIONGOZI WANORUMBANA KWA TAMAA YA KUGOMBEA MADARAKA, MALI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:03 AM
Kiongozi wa kimila wa Kabila la Wangoni, Julius
John (kulia) akimkabidhi siraha za jadi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
katika mapokezi Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma. Siraha ahizo ambazo ni ngao,
fimbo, rungu na shoka ni kwa ajili ya kumpa uwezo wa kupambana na mafisadi na
wengine wote wanaoitakia nchi mambo mabaya. Katikati ni Mbunge wa Jimbo hilo,
Jenista Mhagama.
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi
wa Kimila wa Kabila la Wangoni, Julius John (wa pili kushoto), Katibu wa Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk. Asha Rose Migiro (kulia) pamoja na Mbunge
wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (wa pili kulia) baada ya kukabidhiwa
siraha za jadi.
Kinana akiangalia ngoma ya asili
Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama
(katikati) akishangiliwa na wananchi baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana (hayupo pichani) kumsifia kuwa ni kiongozi bora na kumfananisha na chuma
cha Mjerumani wakati wa mkutano uliofanyika nyumbani kwa Balozi Said Issa mjini
Peramiho, mkoani Ruvuma, akiwa katika muendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa
chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto),
akinywa chai na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (kulia) nyumbani
kwa Balozi wa Shina CCM namba 28, Said Issa (katikati) mjini Peramiho
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
(kushoto) akishiriki kupiga gita wakati bendi ya Ngomande ikitumbuiza wakati
Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipowasili
mjini Peremiho, mkoani Ruvuma. Anayecheza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho,
Jenista Mhagama.
Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: