MAYWEATHER ULINGONI LEO KATIKA PAMBANO LA KWANZA TANGU ATOKE JELA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 5:14 AM
BAADA ya mwaka mmoja nje ya ulingo na miezi miwili
jela, bondia bora kabisa duniani, Mmarekani Floyd Mayweather anarejea ulingoni
usiku wa leo kwenye ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas.
Pambano lake la mwisho alipigana na Miguel Cotto na
kushinda na leo atapambana na Robert
Guerrero, ambaye mwenyewe anajiita The Ghost, yaani Mzimu katika uzito wa Welter
Raundi 12.
Yuko sawa: Floyd Mayweather
alionekana yuko sawa wakati wa kupimzika uzito
Utaona: Mabondia hao
wakitambiana wakati wa kupima uzito
Hunitishi: Mabondia
wakitunishiana vifua wakati wa kupima uzito
Pambano la Mayweather na Guerrero litaonyeshwa live na
BoxNation kupitia Sky Channel 437 na Virgin Channel 546 kuanzia saa 7.30 usiku
wa leo sawa na saa 9:30 kwa saa za Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: