| Mheshimiwa Kaluwa (kushoto), na viongozi wenzake hao wakiimba wimbo maalumu kabla ya kufungua mkutano huo. |
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ilala, Alfred Tuliko (katikati), akihutubia kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa imbo la uchaguzi la Segerea wametakiwa kuacha makundi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika mapema hivi karibuni.
Mwito huo umetolewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonnah Kaluwa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kipawa.
"Uchaguzi mkuu umekwisha pia sasa ni wakati wetu sisi vijana kujipanga badala ya kutofautiana sisi kwa sisi jambo linaloweza kudhoofisha chama chetu" alisema Kaluwa.
Alisema vijana n nguzo ndani ya chama hivyo wakiyumba na chama chote ktayumba na kutoa mwanya kwa wapinzani hivyo aliwataka vijana hao kuipanga na kuhakikisha viti vyote vya uongozi vinanyakulia na CCM katka uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Aliwataka vijana hao kuungana ili waweze kunufaika na mradi wa Youth in Action ambao ni kwaaili ya vijana wote wa Jimbo hilo bila ya kuali itikadi ya vyama vya siasa.
Meneja wa mradi huo Haj Mangara alisema kwa kuanza wataanza na vijana 1000 ambao watakuwa kwenye makundi ya vijana 100.
"Tuna kuwa na vijana katika makundi ya watu 100 ili kurahsisha utendaji wa kazi na kadri mafanikio yatakapo kuwa yakionekana ndipo tutakapo ongeza vijana zaidi" alisema Mangara.
Mratibu wa Mradi huo Regina Ogwal amewataka wasichana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia mradi huo ambao upo kwa ajili yao.
0 comments: