Askari Polisi akiwatuliza 
wanafunzi  wa Shule ya Msingi Tabata 
Kimanga, Dar es Salaam, waliofika kuwasikiliza wananchi waliokuwa wakitoa maoni 
yao mbele ya wajumbe wa  Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba, iliyofika maeneo hayo leo.
 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya 
Sekondari ya Magoza Tabata, wakijaza fomu kwa ajili ya kutoa maoni yao, mbele ya 
wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, waliofika maeneo ya Tabata Kimanga, Dar 
es Salaam jana, kusikiliza maoni ya wananchi leo.
Baadhi ya wajumbe wa Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba, wakisikiliza maoni ya wakazi wa Tabata Kimanga, Dar es 
Salaam, wakati wajumbe hao walipofika maeneo hayo leo kuchukua maoni ya 
wananchi. 
Mwananchi wa Tabata Kimanga, Makame Mpate, akitoa 
maoni yake mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyofika maeneo 
hayo jana kuchukua maoni ya wananchi.
Wananchi waliofika kwenye 
mkutano wa kukusanya maoni ya Katiba mpya, wakisikiliza maoni yaliyokuwa 
yakitolewa na baadhi ya wananchi, mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya 
Katiba kwenye mkutano huo.
Mwananchi wa 
Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Mchungaji Gordon Kangaulaya, akitoa maoni yake 
mbele ya wajumbe wa Kamati ya Katiba, iliyofika maeneo hayo leo kusikiliza maoni 
ya wananchi kuhusu katiba mpya. 
0 comments: