
Leo hii
nimepata muda wa kutafakari nguvu au uzito wa maneno yanayopatikana
katika wimbo wa taifa letu. Muktadha mkubwa katika wimbo huu ni maombi
kwa Mungu kuibariki Afrika hali kadhalika kuibariki Tanzania.
Kuna ombi
la kuomba kwa Muumba alete baraka kwa viongozi, maombi ya kuomba
hekima, umoja na amani kama ngao kwetu Waafrika na watu wake.
Sehemu ya
pili ni maombi tena kwa Mungu aibariki Tanzania, inafuatiwa na kumsihi
Alie juu kudumisha uhuru na umoja kwa wanawake, wanaume na watoto.
Kibwagizo
cha wimbo wa Taifa kimejikita kuomba baraka kwa Afrika, Tanzania na
baraka kwa watoto wa Afrika vilevile baraka kwa watoto wa Tanzania.
Naomba
msomaji wa makala hii ujikite katika kutafakari uzito wa maneo yenye dua
kwa Muumba wa mbingu nan chi adumieshe uhuru na umoja ukiwa ni msingi
wa ulinzi wetu. Tukumbuke ngao ni moja ya silaha za kijadi toka nyakati
za kale ambazo wazee wetu walishika kujilinda dhidi ya mashambulizi ya
mikuki au mishale iliyokuwa inarushwa na maadui kwa nia ya kuwadhuru au
kuwaua kabisa. Lengo la kushika ngao kwa mpigananji ni kujikinga dhidi
ya mishale, mkuki au silaha yoyte inaoweza kuondoa uhai au kuleta
majeraha makubwa katika mwili wa mshika ngao.
Tukiwa
tumetimiza miaka 55 ya uhuru na miaka 54 ya Jamhuri, ni vema
tukatafakari kwa pamoja na kwa kina, kwa marefu, kwa ,apana hali
kadhalika kwa kimo; je, sisi Watanzania bado tunajiona wamoja dhidi ya
maadui zetu wa ndani nan je ya mipaka yetu?
Wanaume,
wanawake na watoto tunahusika kujenga Tanzania kuanzia ngazi ya familia,
jamii na taifa la Tanzania kwa sisi tulio ndani ya mipaka ya nchi hii
na kwa walio nje ya nchi. Utaifa wetu unakuwa na nguvu sana pale ambapo
UMOJA unakuwa na nguvu kubwa bila kujali kama mimi naishi kijijini
Nyamatala wilayani Kwimba au kama wewe msoji uko Atlanta, nchini
Marekani.
Rai yangu
ni kuwa umoja na amani ni silaha wa kujilinda dhidi ya maadui hali
kadhalika ni silaha za kutuunganisha ili tusonga mbele kimaendeleo kama
famila ya akina baba, akina mama na watoto.
Wimbo wa
Taifa umejikita kutamka baraka kwa viongozi wetu. Dhamana ya kutuogoza
tumeiweka kwao kuanzia ngazi ya wenyeviti wa vitongoji kwa serikali za
mtaa mpaka ngazi ya kitaifa inayoongozwa na Mheshimiwa Rais na ambae ni
mkuu wa nchi na kiongozi wa mhimili wa utawala (executie branch) ambae
ana wasaidizi kupitia baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wiliaya mpaka
ngazi ya tarafa . Je, tunatamka nini kwa viongozi wetu, lawama kwa
changamoto wanazozipitia au kuwashauri kwa nia njema ili kutuongoza
vyema?
Kwa wale
tunapata fursa ya kwemda kwenye nyumba za ibada tutakuwa tumewahi kusoma
hekima za mfalme Sulemani mwandishi wa kitabu cha methali. Mfalme
Sulemani amenukuliwa akisema mauti na uzima upo katika nguvu ya ulimi na
kwa wale wanaoupenda watakula matunda yake.
Jambo
jema la kutia moyo ni kuwa viongozi wengi wa kitaifa wenye nafasi ya
kutuunganisha waliapa kwa kushika vitabu vya dini ambazo zina amini
kwenye kutuunganisha kama jamii ya amani dhidi ya chuki. Je, sisi tulio
na nafasi ya kuongoza, tunatamka nini kama viongozi, hayo tunayonena ni
baraka kwa taifa hili au kinyume chake? Tuliopa ee Mungu nisaidie,
tuliomba msaada wa kutuunganisha ile tusonge mbele, au hata hatukumbuki
kama tuliomba msaaada kwa Alie juu?
Ni maombi
yangu turejee upya uzito wa mistari ya wimbo wa Taifa wa kuomba baraka
na kuwabariki viongozi wetu kama msingi wa umoja na amani yetu kwa ajili
ya maendeleo endelevu ya Tanzania tunayoitaka.
Mungu ibariki Tanzania, Wabariki viongozi wetu….(P.T)
Mungu ibariki Tanzania, Wabariki viongozi wetu….(P.T)
0 comments: