Saturday, April 18, 2015

WAZIRI WA FEDHA NA UJUMBE WAKE WAKUTANA MKURUGENZIMTENDAJI WA KUNDI LA AFRIKA


Displaying DSC_5293.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiandika maelezo na hoja kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika ( Afrika Group 1 Constituency) Bi.Chileshe Mpundu Kapwepwe(hayupo kwenye picha). kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.
Displaying DSC_5299.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania katika majadiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika ( Afrikca Group 1 Constituency)Bi.Chileshe Mpundu Kapwepwe(hayupo kwenye picha). kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatiwa na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na kufuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.Pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.(P.T)
Displaying DSC_5300.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akielezea jinsi Tanzania inavyotekeleza sera zilizowekwa na mashirika ya kimataifa kama (WB) na (IMF) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika ( Afrikca Group Constituency)Bi.Chileshe Mpundu Kapwepwe.kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile.
Displaying DSC_5302.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akisikiliza kwa makini maswali aliyokuwa akiulizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Afrika ( Afrikca Group Constituency)Bi.Chileshe Mpundu Kapwepwe hayupo kwenye picha.Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile.
Displaying DSC_5326.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Ngosha Saidi Magonya, Kamishna wa Fedha za nje.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili.
Displaying DSC_5327.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akisikiliza kwa makini maelezo na msimamo wa uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) hawapokwenye picha.Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington DC. Mhe.Liberata Mulamula.
Displaying DSC_5328.JPG
Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni za mfuko wa Changamoto za Milenia, Bw. Kamran Khan wa katikati akitoa maelezo na msimamo wa mfuko wa Changamoto za milenia. Wengine ni viongozi wa mfuko wa changamoto za Milenia wakiongea na ujumbe wa Tanzania ( hawapo kwenye picha).
Displaying DSC_5329.JPG
Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni za mfuko wa Changamoto za Milenia, Bw. Kamran Khan akizungumza na ujumbe kutoka Tanzania na kutoa maelekezo ya jinsi ya kuutumia mfuko huo nchini Tanzania.
Displaying DSC_5333.JPG
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) hawapo kwenye picha. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Ngosha Saidi Magonya, Kamishna wa Fedha za nje.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa.(Picha zote na Ingiahedi Mduma- Washington DC.)

No comments:

Post a Comment