Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
8:02 AM
Mwaka 335-280
nchini Ugiriki kabla ya kuzaliwa kwa Kristo alitokea mwanasayansi
nchini humo aitwaye Herophilus, huyu ndiye mtu wa kwanza kujenga mafunzo
juu ya maumbile ya mwanadamu, kitaalamu 'Anatomy'Mwanasayansi huyu
ndiye baba wa somo la Anatomy yaani maumbile ya mwili. Huyu ndiye
aliyebainisha kuwa ndani ya mwili wa mwanadamu kuna damu na si hewa. Kwa
kutumia taaluma hiyo alianza kujifunza kufanya upasuaji wa maiti ili
kujifunza na kuzifahamu sehemu zinazounda mwili, ikiwamo ngozi, mishipa
ya damu, ya fahamu, misuli na ogani za mwilini.Kutokana na mafanikio
yake na umuhimu wake kuelekea katika fani ya tiba, somo la upasuaji wa
maiti ulianza kutumika duniani katika vyuo vya tiba.Ingawa palitokea
upinzani wa kidini wakitaka jambo hili lizuiliwe, paliwekwa taratibu
maalumu zilizokubalika na kusimamiwa kisheria.
Upasuaji maiti
Wanafunzi
wote wanaosoma sayansi ya tiba duniani mwaka wa kwanza hufanya upasuaji
wa maiti ili kujifunza maumbile ya mwanadamu yalivyo, hii husaidia
katika fani ya utabibu kwani maiti hizo zinakuwa ndiyo mgonjwa wa kwanza
wa mwanachuo.
Mwaka
1831, ilihalalishwa kisheria kwamba miili iliyokosa ndugu au
kutotambulika, itumike kwa wanafunzi wa chuo wanaosomea fani ya sayansi
ya tiba.
Kwa bahati mbaya hapo baadaye ikaonekana maiti za namna hiyo si rahisi kuzipata huku mahitaji yakiongezeka.
Mwaka
1839 huko Chicago, Marekani ulianzishwa utaratibu maalumu wa kuomba watu
kujitolea miili yao pale watakapofariki ili itumike kwa ajili ya
kujifunzia maumbile ya mwanadamu. Zikawekwa kanuni na sheria kuhusu
muundo mzima wa jambo hilo bila malipo. Taratibu hizo zilirithiwa sehemu
mbalimbali duniani lakini hufanyika kwa usiri mkubwa.
Cadaver ni nini?
Ni maiti
za watu ambazo hutumiwa na wanafunzi wa vyuo vya tiba kwa ajili ya
wanafunzi kujifunza na kuona maumbile ya mwili mzima. (MWANANCHI)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: