Askari Polisi akiwatuliza
wanafunzi wa Shule ya Msingi Tabata
Kimanga, Dar es Salaam, waliofika kuwasikiliza wananchi waliokuwa wakitoa maoni
yao mbele ya wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, iliyofika maeneo hayo leo.
Baadhi ya wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, wakisikiliza maoni ya wakazi wa Tabata Kimanga, Dar es
Salaam, wakati wajumbe hao walipofika maeneo hayo leo kuchukua maoni ya
wananchi.
Mwananchi wa Tabata Kimanga, Makame Mpate, akitoa maoni yake mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyofika maeneo hayo jana kuchukua maoni ya wananchi.
Wananchi waliofika kwenye mkutano wa kukusanya maoni ya Katiba mpya, wakisikiliza maoni yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wananchi, mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment