-Awataka watanzania kutoka kwa wingi kupiga kura kumchagua Dkt Samia Suluhu,Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCM.
Latest Articles
DCI MSTAAFU BALOZI ADADI RAJAB OCTOBA 29 TUJITOKEZENI KWA WINGI KUPIGA KURA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 4:33 AMWAKILI MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KUFUNGUA KESI KWA NIABA YA WANANCHI KUHUSU TOZO DARAJA LA KIGAMBONI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:40 AM
Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mohamed Majaliwa
WAKILI wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mohamed Majaliwa amesema kwa niaba ya wananchi wa Kigamboni anakwenda kufungua kesi ya Kikatiba kuomba Mahakama itoe tamko kwamba kulipa tozo la Daraja la Kigamboni ni kinyume cha Katiba.
Wakili Majaliwa amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mchakato wa kufungua shauri la Kikatiba Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Amesema wamefikia hatua hiyo, baada ya kutumia mbinu mbalimbali ya kumaliza tatizo hilo lakini imeshindikana, wameamua kwenda kisheria zaidi ili kuondoa changamoto hiyo.
"Tunakwenda kufungua kesi kwa kuomba Mahakama itoe tamko tu kwamba kitendo cha wananchi wa Kigamboni au mwananchi yeyote kutoka nje ya Kigamboni kutaka kuvuka kuingia kulazimika kulipa tozo ya daraja ni kinyume na Katiba,"
"Na hasa kuzingatia juzi wastani wa mwezi mmoja umepita nilikuwa nimefuatilia uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya miaka 25 mbele sijaona nafuu kwa watu wa Kigamboni kuondosha tozo zile, "Amesema Wakili Majaliwa.
Amesema utaratibu unaoendelea wa tozo hizo, unakizana na sheria zenyewe, sheria ambazo zinatumika kutoza tozo zipo za aina mbili, The Road Tolls (Fees) Regulations, 1985 (Kanuni ya tozo za barabara) na The Road and Fuel Tolls Act (Sheria ya tozo za barabara na mafuta).
"Ukizisoma sheria hizi mbili kwa pamoja kwa ujumla wake, mimi mwananchi wa Kigamboni nikitumia daraja kwa kuvuka kwa daladala au gari yangu binafsi naangukia katika kulipa kodi mara mbili,"amesema
read moreMGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa rai kwa vijana nchini wasikubali kudanganyika ili kuchafua amani ya nchi.
Akizungumza leo katika viwanja vya TANESCO -Buza villivyopo Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam akihitimisha mikutano yake ya kampeni za uchaguzi mkuu, Dk. Samia ametumia nafasi kuwaeleza vijana umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini.
Amesisitiza kwamba Tanzania ni eneo sahihi kwa vijana kuishi tofauti na maeneo mengine Afrika, hivyo amewataka wasikubali kufanganywa kwa namna yeyote ili kuvuruga amani ya nchi yao.
"Hapa mpo kwenye nchi yenye jina, yenye sifa zake, yenye kuendeleza watu wake. Msidanganywe wale ambao wapo nje wasiwadanganye.
“Hapa mpo pazuri kweli kweli.Niwahakikishie vijana wa Tanzania, hawa wazee wenzangu wanaelewa. Vijana wa Kitanzania msidanganywe, ukichukua Afrika Mashariki, Kusini na Kati, Tanzania ni pepo.Nchi yetu iko salama”
Akisisitiza zaidi Mgombea Urais Dk.Samia amesema "Mkipata fursa kuingia kwa majirani zetu, mtaona vijana wenzenu wanavyokula ngumu. Mtasema mnataka kurudi kwenu."
Amewakumbusha kuwa vijana ndio wanategemewa kukabidhiwa nchi kuiendesha kama inavyoendeshwa bila kudanganywa.”Katika kuongoza nchi, taifa limeweka mifumo mizuri ya kidemokrasia kwa kuchaguana kila baada ya miaka mitano.”
"Tulizeni munkali, nchi hii ni mali yenu, hakuna mwenye cheti anayesema nchii hii ni mali yangu. Sisi tunawakilisha wananchi, wananchi ndiyo nyinyi.Hakuna mwenye miliki ya wananchi, wananchi ndiyo nyinyi.
“Tumepeana tu majukumu, niwaombe sana vijana msiharibu nchi yenu. Fuateni serikali yenu inavyowaambia, fuateni katiba yenu inavyowaelekeza," amesema Dk.Samia.
Pamoja na hayo ametoa mwito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kupigakura kwani ndiyo haki ya msingi kidemokrasi.
“Hakuna mfumo uliowekwa kuhusu siasa safi kwani siasa safi ni kuhakikisha nchi na wananchi wapo salama ikiwemo kujumuishwa katika maamuzi.
“Serikali imekuwa ikiunda kamati kukusanya maoni kuhusu masuala mbalimbali yenye kuhusu maendeleo ya nchi.Hata panapotokea mazonge kwenye nchi tunaunda tume kuja kuwauliza, mnatoa maoni yenu. Hiyo ndiyo siasa safi.”
Ameongeza kuwa “Mnapokerana mnaitana kuzungumza, tuyazungumze, tuelewane, twende pamoja hiyo ndiyo siasa safi.”Amesema Dk.Samia na kuongeza hayo ndiyo mambo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliyokuwa akiyasimamia ambapo serikali zote za CCM zimekuwa zikitekeleza.
MOHAMED ABDALLAH: MTAMBILE YAJAA FURAHA NA IMANI KWA CCM
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:31 AMWATENDAJI WA UCHAGUZI WAKUMBUSHWA KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:16 AMMjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira amewakumbusha watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo kushirikiana na Wanahabari ili wananchi waweze kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi.
BENK YA NMB NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ZAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA KWA WATEJA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:06 AMUjumbe kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAG) ukiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno, umetembelea makao makuu ya Benki ya NMB na kufanya kikao na uongozi wa benki hiyo ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna.
Kikao hicho kilichofanyika katika makao makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, kikilenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili, hususan katika kubadilishana uzoefu na mbinu bora za utoaji wa huduma kwa wateja.
Ujumbe wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo Bw. Ipyana Mlilo – Mkurugenzi Msaidizi Uratibu, Bi. Leila Muhaji – Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bw. Juma Mziray – Afisa TEHAMA Mwandamizi, na Bw. Nyamhanga Nyamhanga – Wakili wa Serikali.
Kupitia mazungumzo hayo, pande zote mbili zilitambua umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na binafsi katika kukuza ufanisi wa utoaji huduma na kuleta maendeleo jumuishi.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuimarisha utawala bora na kuhimiza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
read more
MISS WORLD NA MISS AFRICA WATEMBELEA WODI YA NJITI PAMOJA NA DORIS MOLLEL FOUNDATION
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 5:54 AM Wameguswa na kazi kubwa inayofanywa kuwahudumia watoto njiti na wamepongeza juhudi zinazofanyika na kuahidi kuchangia vifaa tiba na kusaidia hospitali nyingine zaidi kwenye maeneo yasiyofikiwa.

































.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)





