Zawadi
mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha Michuano ya Soka Jimbo la Temeke,
Mtemvu Cup, vikiwa tayari wakati wa kukabidhi jezi, kwa timu
zinazoshiriki michuano hiyo, kwenye viwanja vya Chuo Cha Bandari,
Temeke jijini Dar es Salaam.
Vijana
wa hamasa wakishangilia wakati wa shamrashamra za uzinduzi wa michuano
hiyo kenye Uwanja wa Chuo Cha Bandari, Dar es Salaam.
Wasanii wa kikundi cha Machozi cha jimboni humo, wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo
Mbunge
wa jimbo la Temeke Abbas Mtemvu(katikati[) akivishwa nyoka na wasanii waliocheza
ngoma ya majoka, wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo,kushoto ni Noeli Salehna kulia ni Sharifu Kussa
Mbunge wa jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akivishwa nyoka na wasanii
waliocheza ngoma ya majoka, wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo
Msanii
wa Kikundi cha Mapambano Theatre cha temeke, Helen John akionyesha
uhodari wake wa kucheza hukuwa akiwa amejipamba kwa nyoka, wakati wa
uiznduzi wa michuano hiyo.
Msanii wa Kikundi cha Mapambano Theatre cha temeke, Helen John
akionyesha uhodari wake wa kucheza hukuwa akiwa amejipamba kwa nyoka,
wakati wa uiznduzi wa michuano hiyo.
Mwenyekiti
wa CCM, wilaya ya Kinondoni Salum Madenge (kushoto) akibadilishana
mawazo na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu (wapili kulia), wakati wa
uzinduzi wa michuano hiyo .Watatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya
ya Temeke, Yahya Sikunjema.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema (wa
pili kulia), akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa CCM Kata ya
Azimio, Essa Uswege kwa ajili ya mashindano ya Mtemvu Cup
yaliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jioni. Kulia ni Mbunge wa
Temeke, Abbas Mtemvu aliyeanzisha mashindano hayo na kushoto ni Diwani
wa Kata ya Azimio, Hamisi Mzuzuri.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema, akimkabidhi vifaa vya michzo,
Diwani wa Kata ya Miburani, Juma Nkenga, wakati wa uzinduzi wa michuano
ya soka jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, kwenye Viwanja vya Chuo
Cha Bandari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema, akimkabidhi vifaa
vya michzo, Diwani wa Kata ya Kurasini, Wilfred Kimani, wakati wa
uzinduzi
wa michuano ya soka jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, kwenye Viwanja
vya Chuo Cha Bandari jijini Dar es Salaam. Timu kutoka kata zote za
jimbo hilo kila maja imepewa vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na jezi na
mipira.
Mke wa Mbunge wa Temeke, Mama Mtemvu (kushoto) akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo
Msanii anayetamba kwa jina la Msagasumu, akihamasisha vijana kwa nyimbo zake, wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akiwasalimia wachezaji wa timy ya Yombo Vituka kabla ya kuanza kwa mashindano hayo dhidi ya timu Temeke Kata ya 14. |
Kipa
wa timu ya Kata ya 14, Frank Ahmed akiokoa hatari golilini wakati
mshambuliaji wa timu ya Yombo Vituka, Seif Ally alipotaka kupachika bao,
wakati wa mechi ya fungua dimba ya Michuano ya Soka Jimbo la Temeke,
Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es
Salaam. Katika mechi hiyo timu hizo zimetoshana nvugu kwa kufungana bao
1-1.
Mchezaji
wa timu ya Yombo Vituka Seif Ally (kushoto) akiumiliki mpira huku
akiandamwa na mchezaji Charles Magige wa timu ya Kata ya 14, wakati wa
mechi ya fungua dimba ya Michuano ya Soka Jimbo la Temeke,
Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es
Salaam. Katika mechi hiyo timu hizo zimetoshana nvugu kwa kufungana bao
1-1.
Mchezaji
wa Yombo Vituka Brighton Sapa (kushoto), akipambana na mchezaji wa
timu ya Kata ya 14, Rashid Kapate, wakati wa mechi ya fungua dimba ya
Michuano ya Soka Jimbo la Temeke,
Mtemvu Cup 2015, kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es
Salaam. Katika mechi hiyo timu hizo zimetoshana nvugu kwa kufungana bao
1-1. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment