▼
Mabakuli
na vikombe ambavyo vitakuwa vikitengenezwa katika Kiwanda cha Gereza
Kuu Ukonga. Vifaa hivyo mabakuli na vikombe vitatumiwa na Wafungwa
waliopo Magerezani kulia chakula. Katika picha anayeonekana ni Mpiga
picha wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza, Deodatus Kazinja
akiwajibika ipasavyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho, Gereza
Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohudhuria hafla fupi ya
uzinduzi wa Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko, Jijini Dar es Salaam
wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe(hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo
mafupi kwa Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe(wa tatu kulia) kabla ya kumkaribisha rasmi kwa uzinduzi wa
Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko (wa kwanza kushoto) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(katikati) akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha kutengeneza Bakuli na Vikombe
vitakavyokuwa vinatumika na Wafungwa Magerezani kulia chakula(wa kwanza
kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kushoto) akiwaonesha
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam jiwe la
msingi la Jengo la Magereza Duty Free Shop iliyopo Gereza Keko, Jijini
Dar es Salaam(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja. Uzinduzi huo wa Magereza Duty Free Shop umefanyika juzi
katika eneo la Gereza Keko.
No comments:
Post a Comment