MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) AFUNGUA MKUTANO WA WANACHAMA WA TUGHE WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt. Angnes Kijazi (wa pili kulia) akizungumza katika Mkutano wa Wanachama wa Tughe, Tawi la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (pichani hawapo)  uliofanyika Dar es Salaam. Februali 17, 2018 . kushoto ni Mwenyekiti Tughe Mkoa  Dar es Salaam Mziwanda Chimwege na Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Tughe Tawi la Mamlaka ya Hali ya Hewa, Aurelia Mwakalukwa
 Baadhi ya wanachama wakipiga makofi mara alipowasili, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt.  Angnes Kijazi

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt.  Angnes Kijazi (wa tatu kulia) akishiriki kuimba wimbo wa chama hicho kabla ya kufungua Mkutano huo, kuanzia kulia ni Katibu wa Tughe Tawi la Mamlaka ya Hali ya Hewa, Benjamin Bikulamche,  Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Tughe Tawi la Mamlaka ya Hali ya Hewa, Aurelia Mwakalukwa na Mwenyekiti Tughe Mkoa  Dar es Salaam Mziwanda Chimwege
 Baadhi ya wanachama wakishiriki kuimba wimbo wa Chama hicho wakiwa na nyuso za furaha baada ya kuwasili katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt.  Angnes Kijazi
 Mwenyekiti Tughe Mkoa  Dar es Salaam Mziwanda Chimwege (wa tatu kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano huo na ambapo alianza kwa kumshukuru Mungu na kumshukuru,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt.  Angnes Kijazi kwa uchapakazi wake na kuwa makini ambapo kwa nasaha fupi alizozitoa na kwa mara ya kwanza kukutana naye moyoni mwangu nimeridhika naye, hayo yalisemwa na Chimwege.

Ni kiongozi makini na mwenye upendoanawapenda watanzania wote kulingana na Taasisi anayo iongoza na nirudie tena kwa kukushukuru sana na nimshukuru Rais wetu mpendwa kukuchagua wewe, Ndugu wanachama mengi yamekwisha zungumzwa na Mkurugenzi na sipendi kurudia lakini asilimia kubwa mnamwelewa sana kwa asilimi kubwa na nirudie kusema ninamuamini,

Sisi kwa upande wa chama, Mkurugenzi mimi nimechaguliwa Octoba 6, 2017   lakini katika kikao cha uchaguzi nilikua na malengo ya kusaidia juhudi za Serikali na juhudi za Serikali ili zifikie malengo zinahitaji utulivu na amani na kutii sheria bila kikwazo,

Viongozi wengi wanatuzungumza kwamba penye kikwazo wanakubari tuzungumze na mimi niwasihi kwamba pale mnapoona kunakikwazo cha mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu fulani basi fikeni mahali tukayazungumze ili mambo yazungumzike na ninaimani kubwa yatatekelezeka.

 Mkurugenzi sisi kwa upande wetu tunataka tuimarishe Chama cha Tughe Mkoa wa Dar es Salaam na katika kuimarisha tunahitaji tupate jengo ambalo litakalokuwa na hadhi amblo litakuwa na ofisi za Chama cha Wafanyakazi Tughe kama lilivyo la jengo la Mwalimu House lakini pia tuna malengo ya kuanzisha Saccos ya tughe yawanachama katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkurugenzi, Tunawaraka za sheria za wafanyakazi ili wanachama wazijue sheria za kazi na kanuni zake mahali pa kazi ambapo Tughe itakua miongoni ambayoiyakayotoa Elimu au mafunzo kwa wanachama wake na ikiwezekana kwa wafanyakazi kwa ujumla, iwapo kama Taasisi husika na Tughe Mkoa wa Dar es Salaam zitakubariana ili kuleta utulivu na amani sehemu za Kazi.
Mwenyekiti Tughe Mkoa  Dar es Salaam Mziwanda Chimwege (kushoto) akimkabidhi nyaraka, Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt. Angnes
Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Dokt. Angnes katika picha ya pamoja na Viongozi na wanachama wa Tughe Mamlaka ya Hali ya Hewa

0 comments: