AJALI YA NDEGE ZANZIBAR, MARUBANI WAWILI WAFARIKI DUNIA

Ajali ya ndege Zanzibar, marubani wawili wafariki dunia


Marubani wawili wamefariki dunia katika ajali ya ndege ndogo iliyotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar.

Vyombo vya habari vya Tanzania vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, marubani wawili Alfred Mcha (26) na Dominic Bomani (64) wamefikwa na mauti hayo baada ya ndege waliyokuwa wanaifanyia majaribio kuanguka na kuteketea kwa moto.  Habari ya kuanguka na kuteketea kwa moto ndege hiyo imethibitishwa pia na mhandisi mkuu wa kampuni ya Tropical Air, David Kisusi.


uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar

Ndege hiyo 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne ilikuwa ni mali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Tanzania (NIT) na kwamba ilikuweko Zanzibar kwa ajili ya matengenezo.

Kwa mujibu wa David Kisusi, ndege hiyo ilikuwa uwanjani hapo kwa takriban miezi sita ikifanyiwa matengenezo. Habari za kidaktari zinasema kuwa, vifo vya marubani hao vilisababishwa na kukosa hewa safi wakati wa ajali na kuathiriwa na moto mkali.

0 comments: