MWILI WA MAREHEMU LULU SYLVESTER MATTUNDA LEMA WAWASILI KIJIJINI NRONGA KWA AJILI YA MAZISHI

 Marehemu Lulu  Sylvester anatarajiwa kuzikwa Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


 Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga


 




Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo
 Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake  Laura na Hans mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo

 Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza jambo mara baada ya mwili wa  marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema kuwasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema,katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyoitamka "mpaka kifo kitakapo tutenganisha mimi na wewe Lulu",hivyo ahadi hiyo umeitimiza. Profesa Lema
pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana. Wapendwa niseme ni vile tunauona msiba, ila tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu
wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali ,na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba
kuwashukuru sana kwa niaba ya usharika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani
pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali  afya imetoweka na huu mwaka ni mzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.
Waombolezaji wakiwa wamebeba  jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo

0 comments: