KAMPUNI YA BRABVO JOB CENTER YATANGAZA AJIRA KWA WATANZANIA WANAOTAKA KUFANYA KAZI ARABUNI. BAADHI ONDOKA LEO KWENDA SAUDIARABIA

Wakala wa  kampuni ya BRAVO JOB CENTRE Abass Mtevu (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wanaoenda Saudia Arabi


Na.John Luhende 
mwambawahabari
Wakala wa  kampuni ya BRAVO JOB CENTRE Abass Mtevu amesema watanzania wanao sema wananyanyaswa  wanapokwenda kufanya kazi katika nchi za Kiarabu  niwale walioenda kwa njia za panya na hawanavibali vya kufanya kazi .
 
Mtemvu atoa wito huo leo alipo kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa anawaaga wafanyakazi hao waliopitia katika kampuni hiyo walipita katika usaili uliofanywa na kampuni ya BRAVO JOB CENTRE
‘’kuna hisia  kuwa   wanaoenda kufanya kazi Arabuni wananyanyasika  mimi nasema labda hao hawakuenda kwa njia halali sisi katika kampuni yetu ya Bravo Job Centre, watu wote wanaokwenda kupitia kampuni hii hawapati matatizo yoyote tuna vibali vyote na tuna tambulika  na tuna ofisi  Saudia ,Omani na Dubai” alisema Mtemvu.
 
Aidha Mtemvu amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za kazi kwaajili ya kufanyakazi katika nchi za kiarabu na kuweka wazi kuwa watu wanatakiwa ni pamoja na  Mafundi,friji na viyoyozi,mafundi Caterpilar, madactari wa Mifugo,na maafisa Mauzo (sells officer) mafundi umeme, wapishi ,na operator wa mashine na madereva.
 
“Makampuni ya ajira ni mengi nawakaribisha BRAVO  kesho Jumatatu  Chan’gombe waombe kazi na ofisi yetu nyingine iko Benjamini Mkapa Tower tunazo nafasi nyigi “alisema .
 
Kwaupande wake Afisa masoko wa kampuni hiyo Abudallah Ndauya amewataka watanzania kuwa watu wakujaribu na kutoziaacha nafasi  hizi zikapita  kwa kuwa wanao uwezo wa kufanyakazi.

Ramadhani  Kaita ni mmja ya watu walifanikiwa kupata kazi katika kampuni hiyo ,amempongeza Mtemvu kwa kuwaamini na kuwapakazi na leo wanaondoka kuelekea Saudia kwaajili kufanya kazi na amewahamasisha watanzania kufanya kazi , nakuongeza kuwa wataiwakilisha vyema  Tanzania wanakoenda kufanya kazi.

0 comments: