Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana , kulia ni Balozi wa Kuweit nchini Tanzania, Jasem Al-Najem.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo mara alipowasili katika chuo hicho
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kushoto), wakati mmoja wa mwanafunzi wa Chuo hicho, Lenah Sauli alipokua akishona nguo
Mkufunzi Mkuu Msaidizi Regina Makotha (kulia) akizungumza kwa kuwapa ishara yale aliyokuwa akizungumza Waziri Mhagama
Wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu wakiashiria kupiga makofi wakati walipokuwa wakipewa ishara na Mwalimu wao, Mkufunzi Mkuu Msaidizi Regina Makotha (pichani hayupo) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza jambo katika hafla fupi ya kumkabidhi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto) vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni msaada kutoka serikali ya Kuweit, hafla iliyofanyika jana katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana, wakwanza kushoto ni Katibu Muhutasi wa Balozi na wakwanza kulia ni Mkalimani wa Balozi, Abdallah Yahaya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cherehani, Lenah Sauli (kushoto)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimvisha miwani mwanafunzi wa Chuo hicho, Mandela Lamwai ambaye anasomea ufundi umeme
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi
mafuta maalumu ya kujipaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi mwanafunzi wa Chuo hicho, Mandela Lamwai ambaye anasomea ufundi
umeme, wa tatu kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem
KUWAIT YAZINDUA MPANGO KAMILI WA KUWASAIDIA WALEMAVU TANZANIA
Serikali ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake nchini umezindua mpango
kamili wa kuwasaidia watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi
Yombo,uzinduzi ambao ulihudhuriwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem
Al-Najem, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,vijana,Ajira
na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama,Kaimu wa Chuo Bi Maryam, walimu na
wanafunzi wa chuo hiko kilichoanzishwa mwaka 1973 na kutoa mafunzo
mbalimbali kama umeme,ushonaji n.k.
Balozi wa Kuwait Al-Najem katika hotuba yake wakati wa uzinduzi amesema
kuwa mpango huo utagharimu kiasi cha dola laki 5 sawa na shilingi
bilioni 1.1 utaendeshwa nchi nzima kwa awamu kwa kushirikiana na maafisa
wa Serikali ya Tanzania na mashirika yasiyokuwa
ya kiserikali.
Pembezoni mwa uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya siku
ya watu wenye ulemavu duniani, Al-Najem alimkabidhi Waziri Mhagama
vifaa vya walemavu kama viti vya matairi,fimbo,magongo,miwani,vifaa vya
kuwasaidia wenye udhaifu wa kusikia na mafuta ya
kujipaka kwa walemavu wa ngozi albino huku akiahidi kuchangia vifaa ya
upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa katika Taasisi ya Mifupa MOI.
Kwa upande wake Waziri mwenye dhamana Mhe. MHAGAMA amesema kuwa Tanzania
itaendelea kutekeleza maazimio ya kimataifa kuhusu walemavu huku
akiyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na sekta binafsi kuiga
mfano wa Serikali ya Kuwait, watu wake na Ubalozi wake
katika kuwasaidia walemavu nchini.
Waziri Mhagama ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa misaada hii na kuuomba
Ubalozi kusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili Chuo
cha Ufundi Yombo kama vile uchimbaji wa kisima na makazi kwa wanafunzi
walemavu.
0 comments: