JAFO MGENI RASMI KONGAMANO LA UWAJIBIKAJI KWA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NCHINI DEC 5-6

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano  la uwajibikaji kwa mamlaka za  Serikali za mitaa nchini linalotarajiwa kufanyika kuanzia kesho Desemba 5-6,2017 katika hoteli ya Ramada iliyopo Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo  linatarajiwa kuwa na washiriki  zaidi ya 120 ambao ni pamoja na Mameya/Wenyeviti wa Halmashauri pamoja na Wakurugenzi Watendaji kutoka Halmashauri zaidi ya  120 kote nchini.
Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WAJIBU (Wajibu Institute of Public Accountability)  Lodovick Utouh amesema kuwa tayarai maandalizi yote yamekamilika huku washiriki mbalimbali tayari weanza kuwasili.
“Kongamano hili linatarajiwa kufunguliwa na mgeni rasmi Waziri Mwenye dhamana Mh. Suleiman Jafo.  Kongamano ili pia hadi sasa tayari Mameya  50 na Wakurugenzi Watendaji 70 wamethibitisha kuhudhuria .
Mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina  na washiriki wa kongamano hili. Miongoni mwa mada hizo ni pamoja na  mkakati wa Serikali  ya awamu ya tano wa utekelezaji wa Sera yaa viwanda- ISDP, Mpnago wa pili wa Maendeleo 2016/17-2020/21 na mada zingine nyingi” alieleza Lodovick Utouh.
Utouh aliongeza kuwa, kongamano hilo linatarajia kutoa taswira  katika majadiliano na kufikia maazimio juu ya mbinu zitakazotumika kufikia Tanzania ya uchumi wa Kati wa viwanda na kuongeza uwajibikaji wa Serikali za Mitaa nchini katika usimamizi wa rasilimali za Umma.
Taasisi hiyo ya WAJIBU ambayo ni taasisi (think-tank organization) ya uwajibikaji wa umma iliyoanzishwa mwaka 2015 kwa lengo la kutengeneza mazingira ya kukuza uwajibikaji na Utawala bora hapa nchini.
Aidha,  kwa  kutambua  nafasi ya kuongeza uwajibikaji na kuchangia maendeleo ya Taifa la Tanzania, Taasisi ya WAJIBU kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia mradi wa (GFC) wamekuja na kongamano hilo lenye maudhui “Ushiriki na Uwajibikaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ujenzi wa uchumi wa kati kupitia viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WAJIBU (Wajibu Institute of Public Accountability)  Lodovick Utouh akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani ) wakati wa kutangaza kongamano hilo linalotarajiwa kuanza kesho Desemba 5-6,2017.

0 comments: