NYALANMDU AUNGANA NA VIONGOZI WA CHADEMA, MAZISHI YA MCHUNGAJI LOOKA MUSHI, ALIYEKUWA MKUU WA JIMBO WA CHAMA HICHO

 Waziri Mstaafu wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, (kushoto), akiungana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe (Watatu kushoto) na viongozi wengine wa chama hicho, kwenye mazishi ya Mkuu wa jimbo mstaafu wa chama hicho, marehemu Looka  Mushi, yaliyofanyika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Novemba 17, 2017. Nyalandu ambaye pia alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, alijivua vyeo vyote ikiwemo uanachama wa CCM na sasa anasubiriwa kujiunga rasmi na CHADEMA.
 Mheshimiwa Mbowe, akiweka shada la mauwa kwenye kaburi la marehemu, Looka  Mushi, yaliyofanyika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Novemba 17, 2017.
  Mheshimiwa Mbowe, akitoa heshima mbele ya kaburi la marehemu Mushi wakati wa mazishi yake.
 Mheshimiwa Nyalandu akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.
   Mheshimiwa Mbowe, akitoa heshima zake mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mushi.


 Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Mhe Freeman A. Mbowe (Wapili kushoto) akiwa na Mbunge wa Arusha mjini,Mhe Godbless Lema , Waziri Mstaafu wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi,Uenezi na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema, kabla ya kuelekea kwenye msiba wa Mkuu wa jimbo mstaafu, Mchungaji Looka Mushi huko jimboni Hai, Novemba 17/11/2017




0 comments: