CHAMA CHA WAKUNGA TAWI LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (MNH) CHATOWA HUDUM BURE KWA WANANCHI

  Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Flora Kimaro (wa kwanza kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara Uuguzi na Mazingira wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona  wakati wa maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika eneo la Hospitali hiyo Dar es Salaam. wa pili kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Tawi la Wakunga Muhimbili (MOI, MNH NA JKCI) (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

 Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Flora Kimaro (wa katikati) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha TAMA Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Priscillah Kinyamagoha na Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona
 Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimlili (MOI), Flora Kimaro akitia saini katika kitabu cha wageni wakati alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Wakunga katika Wiki ya Unyonyeshaji (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo alikuwa Mgeni rasmi
 Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimlili (MOI), Flora Kimaro (katikati) akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kushoto ni Mkuu wa Idara Uuguzi na Mazingira wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona na kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha TAMA Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Priscillah Kinyamagoha 


 Baadhi ya viongozi Wakipiga makofi mara baada ya Mgeni rasmi kukata utepe wakati wa Maadhimisho ya  Uzinduzi wa wa Chama Cha Wakunga


 Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Flora Kimaro (wa pili kulia) akiwapungia wananchi waliyojitokeza katika kupata huduma za upimaji wa Afya kwa wananchi bure  katika eneo la maegesho ya magari (OPD) jirani na lango kuu la kutokea nje ya Hospitali hiyo.

Huduma zilizotolewa ni pamoja na: 

a. Upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti

b. Upimaji wa shinikizola damu, sukari, uzito na urefu

c. Upimaji wa virusi vya ukimwi (VVU) kwa hiari

d. Ushauri kuhusu lishe bora 

e. Ushauri kuhusu uzazi wa mpango

f. Elimu juu ya unyonyeshaji sahihi kwa watoto chini ya umuri wa miaka mwili

g. Elimu juu ya afya ya kinywa na meno 

Aidha TAMA Muhimbili inatarajia kufanya kongamano la Kisayansi la wakunga tarehe 7, Agosti 2017 saa tatu asubuhi katika ukumbi wa namba 60 uliyopo eneo la jengo la OPD ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Ukunga na Mazingira ya ndani ya Hospitali hiyo,  Agnes Mtawa.

Maadhimisho ya siku ya mkunga duniani mwaka huu wa 2017, yanabebwa na kauli mbiu isemayo " WAKUNGA, WANAWAKEN FAMILIA NI WASHIRIKA WA KUDUMU" . kuanzia kushoto, Kaimu Mwenyekiti wa Tawi la Wakunga Muhimbili (MOI, MNH NA JKCI), Mwenyekiti wa Chama Cha TAMA Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Priscillah Kinyamagoha, Mkuu wa Jengo la Kliniki za Nje, June Samwel (aliyevaa nyeupe) na kulia ni   Mkuu wa Idara Uuguzi na Mazingira wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona, 

Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Flora Kimaro akihutubia wananchi waliyofika kupata huduma bure wakati wa Maadhimisho ya siku ya mkunga duniani

 Waugizi waliyovalia sare wakiwa na wananchi waliyojitokeza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani kupata kuhuma bure
 Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Gredisia Kessy (kushoto) akichukua vipimo vya presha toka kwa mmoja wa wananchi (kulia) waliojitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.


 Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mwanne Satara (kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa Maadhimisho ya siku ya mkunga duniani yaliyofanyika katika Hospitali hiyo, kuanzia kulia ni, Afisa Munguzi Msaidizi, Ester Mwambogoja na wakatikati ni Afisa Muuguzi Msaidizi, Gudila Mambacho

 Afisa Muuguzi Msaidizi, Mshauri Nasaha na Mpimaji wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti, Matilda Mriwa (kulia) akizungumza na wananchi waliyofika katika  Maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani na kupata kuhuma bure

 Mgeni rasmi katika picha ya pamoja
 Picha ya pamoja ya wafanyaka 
Mwenyekiti wa Chama Cha TAMA Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Priscillah Kinyamagoh akizungumza na wanahabati

0 comments: