WAYNE ROONEY KUTUA BONGO KESHO AKIWA NA EVERTON


Wayne Rooney
Siku moja baada ya Wayne Rooney kutangazwa kujiunga na Everton FC ambayo ni timu yake ya utotoni akitokea Man United kama mchezaji huru, baadhi ya mashabiki wa soka Tanzania walikuwa wakihisi kwamba huenda Rooney asije Tanzania katika mchezo dhidi ya Gor Mahia.

Wengi walihisi hivyo na kudhani kuwa Rooney anaweza akapewa mapumziko au asije mechi ya Tanzania akaungana na wenzake katika mechi ya pili ya Everton ya maandalizi ya msimu dhidi ya FC Twente ya Uholanzi lakini leo imethibitika kuwa Rooney anakuja Tanzania.

Rooney, juzi alifanya mazoezi na Everton kwa mara ya kwanza, akiwa mchezaji wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na kueleza kuwa ziara ya Everton nchini Tanzania, itamfanya awajue vizuri wachezaji wenzake.

“Hii trip naiangalia kwa uzuri na itakuwa safari sana kwetu na natumaini nitapata nafasi ya kucheza, huwa ni vizuri sana kusafiri na wachezaji wenzako na kutembea sehemu tofauti tofauti, kiukweli sijawahi kufika Tanzania”

0 comments: