MAMA JANETH MAGUFULI ATOA MSAADA MBALIMBALI KWA WAZEE WASIOJIWEZA 400 CHATO MKOANI GEITA

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (katikati) akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato, Winfrida Lawrent (65) kutoka Kata ya Kasenga kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Kilo 4000 Maharage, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (katikati) akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato,  Anatory Bisate (64) (kulia) kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Maharage kilo 4000, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (wa pili kulia) akiwakabidhi kwa pamoja mafuta waakilishi wa Wazee kutoka kata ya Kasenga Anatory Bisate (64) kulia pamoja na Winfrida Lawrent (65) kushoto mara baada ya kuzungumza na wazee 400 katika Ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kula) akiimba pamoja na wanakwaya wa Mwagazege mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mama Janeth Magufuli (kushoto) akiwasili katika eneo la mkutano mara baada ya kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga Chato mkoani Geita.
Mama Janeth Magufuli (wa pili kulia) akiwa na viongozi wengine wa mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakwanza kushoto wakati wa dua kabla ya kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.
Mama Janeth Magufuli (wa kwanza kushoto) akifurahi pamoja na Naibu Waziri wa nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati Kwaya ya Mwakazege ya kutoka Chato ilipokuwa ikitumbuiza kabla ya kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.
Mama Janeth Magufuli akizungumza na Wazee hao
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kushoto) akizungumza na Wazee wasiojiweza zaidi ya 400 kutoka Wilaya ya Chato katika Ukumbi wa Mshikamano Saccos.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa, Wilaya na Chama waliojumuika na Waakilishi wa wazee wasiojiweza zaidi ya 400 Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Wazee wakishangilia wakati wa hotuba ya mgeni rasmi. (PICHA NA IKULU)

0 comments: