WASAUDIA WALIMUHONGA TRUMP MAKUMI YA MAELFU YA DOLA ILI ABADILI SHERIA YA JAST

Magazeti ya nchini Marekani yameandika ripoti inayofichua kwamba watawala wa Saudi Arabia, walitoa hongo ya makumi ya maelfu ya dola kwa Rais Donald Trump wa Marekani ili kumshinikiza ababadilishe sheria ya kukabiliana na waungaji mkono wa ugaidi kwa kifupi JASTA ya nchini Marekani.
Kwa mujibu wa habari hiyo, Aal-Saud walitoa dola laki mbili na elfu 70 kwenye hoteli ya Trump ya mjini Washington ili rais huyo asiwahusishe katika sheria hiyo. Imeongeza kuwa, Aal-Saud wanafanya kila juhudi kwa lengo la kuwalazimisha viongozi wa Marekani kubadilisha sheria hiyo ambayo inasisitizia umuhimu wa kupandishwa katika mahakama za nchi hiyo kila anayeyasaidia kifedha makundi ya kigaidi.
Shambulizi la Septemba 11, 2001 nchini Marekani
Kuhusiana na habari hiyo mtandao wa Shirika la Habari la Russia Today umeandika kuwa, wiki iliyopita Shirika la Mahusiano ya Uma 'MSL Group' liliwasilisha nyaraka mbele ya Wizara ya Vyombo vya Sheria nchini Marekani ripoti ambayo inathibitisha kuhusika Saudia na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani. Habari zaidi zinasema kuwa, zaidi ya dola laki mbili na 90 elfu zilitolewa na Saudia kwa ajili ya kudhamini mahitaji ya chakula na kiasi kingine cha fedha kwa ajili ya eneo la maegesho ya magari katika hoteli ya "Trump International" ambako walikutana viongozi wa hivi sasa na wa zamani wa Marekani kujadili sheria ya Jasta inayoilaumu Saudia kwa kuhusika na mashambulizi hayo ya kigaidi.
Hoteli ya Trump International
Habari zaidi zinasema kuwa, fedha hizo zilitolewa na Saudia baina ya mwezi Novemba 2016 na Februari mwaka huu. Itakumbukwa kuwa, Baraza la Sanate la Marekani limepiga kura ya kubatilisha veto ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo aliyepinga kufuatiliwa wahusika wa mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 nchini Marekani ambapo mashtaka hayo yaliwahusisha moja kwa moja viongozi wa Saudia kwenye mashambulizi hayo. Baraza la Sanate la Marekani limetengua veto ya Obama kwa kura 97 za ndio na moja tu ya hapana. Kwa mujibu wa sheria hiyo ya JASTA, familia za wahanga wa mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani wana haki ya kuomba fidia kutoka kwa Saudi Arabia, kwani watu 15 kati ya 19 walioteka ndege zilizotumika kwenye mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani, walikuwa ni raia wa Saudi Arabia.

0 comments: