MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO KUJENGA MADARASA MATANO MAPYA SHULE YA MSINGI HONDOGO


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo (kushoto) akizungumza jambo mara baada ya kuranya ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John  Kayombo (kushoto) na Afisa Uchumi Mkuu, Yamo Wambura wakikagua majengo ya madarasa ya shule ya msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba wakati wa ziara ya kikazi


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo (kushoto) akizungumza na wanafunzi akiwataka kusoma kwa bidii mara baada ya kufanya  ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John  Kayombo akikagua maendeleo ya wanafunzi wa darasa la nne mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo,  John  Kayombo akimsikiliza kwa makini Mwalimu, Magreth Kapinga mara baada ya ziara ya kikazi katika Shule hoyo ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba


Madarasa manne yaliyoamuliwa kuvunjwa na kujengwa upya madarasa mengine matano katika Shule ya Msingi Hondogo Jijini Dar es salaam


Mwalimu wa Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba, Happness Mashimba akiwa darasani akifundisha somo la Kiswahili darasa la nne kwa kujitolea kipindi hiki cha likizo kama alivyokutwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akifurahia jambo na wanafunzi mara baada ya kufanya  ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John  Kayombo akitoa maelekezo ya kazi mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba



Na Mathias Canal, Dar es salaam 



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo  June 13, 2016 afanya ziara ya kikazi kwa kutembelea shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba Jijini Dar es salaam kujionea hali ya Miundombinu ikiwemo majengo ya shule na ufanisi wa utoaji elimu katika Shule hiyo.


Mara baada ya kuzuru katika Shule hiyo Mkurugenzi Kayombo amebaini kuwapo na ubovu wa madarasa hivyo kuamua kujenga madarasa mengine mapya matano kwa ajili ya wanafunzi kujisomea kwa uhuru na amani shuleni hapo.



Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa utaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.


MD Kayombo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa madarasa hayo yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amesema ujenzi wa madarasa hayo utakuwa wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya ubora wa majengo ya serikali. 

0 comments: