Wananchi
wa kisiwa cha Makoongwe wilaya ya Mkoani Pemba, wakiwa safarini ndani
ya mashua yenye mashine, wakitokea Mkoani mjini kwenda kijijini kwao,
ambapo hayo ndio maisha yao ya kila siku, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Ipo
haja kwa wazazi na walezi, kuwa makini na maeneo wanayocheza watoto wao,
ambapo mtoto ambae hakupatikana jina lake, akikata tawi, alilolikalia
karibu na skuli ya Makoongwe wilaya ya Mkoani
Mwandishi
wa Shirika la Magazeti ya Serikali ofisi ya Pemba Haji Nassor,
akizungumza na Mwenyekiti Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukimwi na Mazingira
JSEUMA, Juma Ali Mati juu ya hatua waliofikia, ndani ya jumuia yao,
kuhusu kuwaelimisha wananchi kupanda miti na kuhifadhi mazingira
Mwananchi
wa shehia ya Mkanyageni wilaya ya Mkoani Pemba alietambulika kwa jina
Seif, akichangia jambo kwenye mkutano wa uhamasishaji wa upandaji miti
uliondaliwa na Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukiwmi na , Mazingira JSEUMA ya
Kisiwani panza, wilaya ya Mkoani Pemba
Wandishi
wa habari kisiwani Pemba, wakisikiliza mada kwenye mmoja ya mikutano
iliofanyika hivi karibuni kwenye uwanja wa Gombani Chakechake Pemba,
ambao uliandaliwa na kitengo cha malaria Pemba.
NA HAJI NASSOR, PEMBA
ABIRIA
waliokuwa wakitokea Unguja, wafanyakazi wa serikali na taasisi binafsi
pamoja na wananchi wengine, juzi walilazimika kusubiri kwa dakika 45,
kwenye eneo la mpakani baina ya wilaya za Mkoani na Chakechake, kufuatia
mti aina ya Muwembe kukatika na kuziba barabara.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi, abiria na wananchi hao walisema, baada ya
kuteremka meli bandari ya Mkoani, walipanda gari za abiria ili kuelekea
kwenye mkaazi yao, ingawa walipofika mpakani walikwama.
Walisema
walikaa hapo tokea majira ya saa 10:30 hadi saa 11:15 ndipo
walipofanikiwa kupita baada ya taasisi kadhaa wakiwemo idara ya misitu
kukakata Muwembe.Walisema kama sio taasisi za serikali zikiwemo KZU,
Idara ya misitu na wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo la Vuleni
kushirikiana wengeutumia hadi saa 1:30.
Mmoja
kati ya abiria aliekuwa akitokea Unguja, Juma Mshihiri Hassan mkaazi wa
Konde, alisema baada ya kufika hapo walishuhudia foleni ya gari zaidi ya
30 na waliarifiwa kwamba barabara imefungika, kutokana na kuanguka
Muwembe katikati.
Nae
Asha Msabaha Himid wa Chasasa alisema, alitarajia akapeleke mzigo kwao,
kisha arudi bandarini kwa vile siku ya pili alikuwa anasafiri, ingawa
kutokana na kuchelewa kuondoka hapo itakuwa vigumu.“Sisi tupo hapa zaidi
ya dakika 45, maana tunakaribia tu na Muwembe huo unanguka, na kuziba
njia yote, maana upande mwengine kuna bonde, hapana pakukimbilia, ingawa
baadae walikuja watu kuukata na kuondoka’’,alisema.
Hata
hivyo dereva wa gari ya Chakechake –Mkoani aliejitambulisha kwa jina
moja la ‘Kipara’ alisema katika kipindi hichi cha mvua, lazima wawe
makini maana miti huunguka kutokana na ardhi kushiba maji.
Kwa
upande wake dereva aliefanikiwa kupenya kwenye eneo hilo la Vuleni na
kisha Muwembe kuanguka, Ali Haji Juma, alisema aliouna umeshainama,
ingawa baada ya nusu saa aliamua kupita salama.“Mimi baada ya kupita
dakika 10 tu, napata taarifa kuwa, umeshanguka na gari zimekwama, ingawa
na juzi nilikwama Ngwachani baada ya Muwembe kuanguka na kuziba
barabara’’,alifafanua.
Hata
hivyo Mkuu wa wilaya ya Mkoani ambae nae juzi ni miongoni mwa wananchi
waliokwama, Hemed Suleiman Abdalla, aliwashukuru watendaji wa taasisi
mbali mbali, kwa umoja na mshikamano wao.
Tokea
kuanza kwa mvua hizi za masika, tayari miti zaidi ya sita imeshaanguka
na kuziba barabara ikiwemo eneo la Ngwachani, Ngezi, Vuleni na Mtambile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: