Waheshimiwa Mawaziri wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Afrika Mashariki unapigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano |
MKUTANO WA 34 WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAMALIZIKA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 5:47 AM
NA MWANDISHI MAALUM
MKUTANO
wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam umefikia tamati. Mkutano huu uliofanyika
katika Hoteli ya Serena umehudhuriwa na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya
Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama, watendaji
mbalimbali kutoka Wizara, mashirika ya umma, Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki, na taasisi mbalimbali za Serikali ndani ya Jumuiya.
Pamoja
na mambo mengine Mkutano huu ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kuandaa agenda
zinazo hitaji maamuzi ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Agenda
hizo zinatokana na taarifa ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali ya
Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya wa mwaka 2015/2016, iliyo andaliwa
na Mkutano wa ngazi ya wataalamu.
Baadhi
ya mambo yaliyopo kwenye taarifa hiyo ya utekelezaji wa maagizo na
maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2015/2016 ambayo imekabidhiwa kwa Baraza la Mawaziri
yanajumuisha mambo yafuatayo;
·
Taarifa ya namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupunguza uagizaji wa
magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya
·
Taarifa ya mapitio kuhusu sekta ya nguo na ngozi juu ya
kuzuia/kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika
na;
· Taarifa ya namna endelevu ya Uchangiaji wa bajeti ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akizungumza na wanahabari punde baada ya mkutano amesema
Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri umekuwa na mafanikio makubwa
kwanza, kutokana na idadi kubwa na yakuridhisha ya wajumbe walioshiriki
Mkutano
kutoka nchi wanachama ,na pili ni kutokana na mafanikio makubwa
yaliyopatika katika kipindi chote cha miaka miwili ambayo Tanzania ilikuwa
mwenyekiti wa Jumuiya hadi sasa inapokabidhi kwa nchi ya Jamhuri ya Uganda.
Mfanikio
yaliyopatikana katika kipindi cha uwenyekiti;
Waziri
Mahiga ameyataja mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka miwili
Tanzania ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya kuwa ni; kuongezeka kwa nchi ya Sudan
Kusini katika Jumuiya, kuboreka kwa mfumo wa elimu kwa ngazi ya elimu ya juu
katika Jumuiya na kupungua kwa vikwazo vya biashara vinavyotokana na vikwazo
visivyokuwa vya kiforodha ndani ya Jumuiya vilivyopelekea kurahisisha na
kuhamasisha baishara katika Jumuiya.
Mkutano
huu wa Baraza la Mawaziri utafuatiwa na Mkutano wa 18 wa Kaiwada wa Wakuu
wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uanaotarajiwa kufanyika tarehe 20 Mei,
2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengine Mkutano wa Wakuu wa nchi unatarajiwa kupokea ripoti ya
usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa.
Tanzania
ilikabidhiwa uwenyekiti wa Jumuiya mwishoni mwa mwaka 2014 katika Mkutano wa
Wakuu wa Nchi uliofanyika Nairobi, Kenya; na ikapewa tena nafasi ya kuendelea
kushikilia kiti hicho mwaka 2015, ambapo mpaka sasa Tanzania wakati inaelekea
kukabidhi nafasi hii ya uwenyekiti kwa nchi ya Uganda, Tanzania imekuwa
mwenyekiti wa Jumuiya kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: