WATOTO YATIMA WATOA NENO KWA WAFADHIKI MKOANI KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma

WATOTO  Yatima na waishio katika mazingira magumu wanaofadhiliwa na Kanisa la Africa, Inland (AIC)  Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Shirika la Compassion wametoa zawadi ya misa maalum ya kutoa shukrani kwa wahisani hao kwa kuonyesha vipaji mbalimbali ambavyo wamefundishwa na walezi wa kanisa hilo kituo cha  973 mkoani hapa kwa kipindi cha zaidi ya Miaka mitatu.

Wakizungumza na Jambo Leo jana baada ya misa hiyo Baadhi ya watoto hao akiwemo Paulo Obed na Aziz Ally kwa nyakati tofauti walisema wanawaombea mungu wahisani hao ambao wamewapa mwanga wa kutimiza ndoto zao za kielimu kwa kuwapa huduma za msingi hasa mahitaji yote ya kielimu na afya pindi wanaposhikwa na maradhi.

Walisema mbali hilo wanahudumiwa chakula ,mavazi na kuwakumbusha walezi na wazazi wasiepuke majukumu yao katika kutoa malezi ya kumcha mungu kwa watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi ambao chimbuko kubwa ni walezi kukwepa majukumu yao.

Walisema kupitia misa hiyo wamebaini vipaji vyao vya uimbaji,ujasiri wa kusimama mbele ya watu wengi na kutoa neno la mungu sanjari na kuwa viongozi wa taifa hilo siku za usoni na kutoa mwito kwa watoto wenzao watumie akili katika kujikwamua na changamoto zinazowakabili na wasitumie vibaya miili yao katika vitendo viovu.

Kwa upande wa walezi wa watoto hao Elizabeth Nyanda alisema wanalea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendela ambao ni yatima na wenye mazingira magumu kutoka familia tofauti tofauti  na wanawapa elimu kuu Nne ambazo ni elimu ya kiroho,kimwili,kijamii ambapo yanampa ujasiri wa kujitegemea kwa kumtanguliza mungu ambaye ndio mwisho la hitaji la wanadamu wema.

Naye Mkurugenzi wa Kituo hicho Robert Chamungu alisema kituo kinapokea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu bila kujali tofauti za udini kwa lengo la kuendelea ndoto zao siku za usoni hali inayochangia wahisani kutoka Compassion na kanisa kutoa huduma za elimu na afya kwa walengwa.

Alisema changamoto kubwa ni baadhi ya mashirika ya kuhudumia watoto kutokushirikiana kwa dhati katika kumkwamua mtoto mwenye hitaji la msingi na kushauri wadau wa watoto wa aina hiyo washirikiane katika kuimarisha ndoto za watoto katika huduma za msingi,hasa alimu,afya,chakula,makazi na mavazi na si kunyang`anyana watoto kwa kutoa huduma zinazofanana.

0 comments: