WATATU MBARONI KWA KUKUTWA NA BOMU MKOANI KIGOMA

Na Mwandishi wetu,kigoma
 
WATU watatu raia wa Nchi ya Burundi waliopewa hifadhi katika Kambi ya
wakimbizi ya Mtendeli Mkoa wa Kigoma,wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
la hapo,kwa tuhuma za upangaji wa magogo  katika barabara kuu  ya
Kigoma ,Kasulu na Kakonko kwa lengo la utekaji wa magari hasa mabasi
ya abiria yaendayo mikoani.

Pia, walipokaguliwa walikutwa na vitu vifuatavyo Bomu moja la kutupwa
kwa mkono(Offensive hand Grenade),Bunduki moja ya bandia,panga
mbili,rungu 3,viatu aina ya raba jozi moja,viatu vya kike jozi
moja,simu aina ya nokia Nne,Tecno tatu,vipodozi vya kike,laptop ,power
benki,saa,sanjari na nguo mbalimbali za kiume.

Akizungumzia  tukio hilo leo mbele ya wandishi wa habari ofisini
kwake kigoma Ujiji,Kamanda wa Polisi Ferdinand Mtui alisema walibaini
hilo baada ya askari polisi waliokuwa katika doria kwenye njia hiyo
yenye mapori makubwa ndipo  waliwakamata watuhumiwa hao ambao walikuwa
kwenye mtego.

Aliyataja majina ya watuhumiwa hao ni pamoja na Hakizimana
David(21),Nepomseni Niogere(25) na Nduwamahoro Justine(20) wote  ni
wakimbizi wanaoishi katika kambi ya mtendeli iliyopo wilaya ya Kakonko
na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Alitoa mwito kwa raia wote wa kigeni  waliopewa hifadhi  katika kambi
mbalimbali za wakimbizi mkoani humo watii sheria,kanuni na taratibu
zote za nchi na waache kujihusisha na vitendo vya kihalifu.

0 comments: