WAKIMBIZI KUPEWA FEDHA UTEKAJI MABASI YA ABIRIA KUISHA KIGOMA?

Na Magreth Magosso,Kigoma

IMEELEZWA kuwa, kitendo cha kuwapatia fedha taslimu badala ya chakula kwa wakimbizi waliohifadhiwa katika hifadhi ya nyarugusu iliyopo wilayani kasulu ,mkoani kigoma, itasadia kupunguza matukio ya ujambazi na utekaji wa mabasi ya abiria kwa kutumia silaha za moto unaofanywa na baadhi ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali za kigoma.

Akielezea hilo,juzi wilayani kasulu ,Kaimu Mkuu wa wilaya Kasulu, Kanali Marco Gaguti alisema kuwa mpango huo utaiwezesha serikali kusimamia kikamilifu masuala ya ulinzi na usalama wa raia wa mkoa wa kigoma kwa ujumla.

Kanali Gaguti alisema  kabla ya utekelezwaji  wa mpango huo wakimbizi wengi walikuwa wanatoka kambini na kuingia mitaani  wakifanya shughuli za vibaruakatika mashamba ya wananchi, ili wapate pesa za ziada na  wengine wakijihusisha na vitendo vya ujambazi .

“ kitendo cha kupewa  fedha taslimu badala ya chakula kutaondoa ulazima wa wakimbizi kwa madai ya  kutoka kambini kwenda nje ya kambi ,ili kununua vyakula tofauti na vile vilivyokuwa vikitolewa kambini, pia utafaidisha wananchi  wanaoishi karibu na kambi , fursa ya masoko kwa mazao ya  chakula kambini humo” alieleza Kanali  huyo.

Mkuu wa Shirika la umoja wa mataifa la mpango wa chakula (WFP) wilayani Kasulu,Saidi Johari alisema  mpango huo ulianza mwezi Desemba mwaka jana na wamebaini faida kubwa kwa wakazi wa kasulu hasa wanaopeleka kuuza mazao  kambini hapo kwenye soko la pamoja ambpao ,bidhaa za vyakula yana mahitaji makubwa.

Mkuu huyo wa WFP wilaya ya Kasulu alisema kuwa pamoja na faida kiuchumi pia umepunguza mzigo wa kazi kwa watumishi wa shirikahilo, ambapo  kwa sasa wana uwezo wa kugwa fedha ndani ya siku chache ambapo huwaulisha fedha  kwa siku tatu badala ya siku 5 hadi 7 nyakati za ugawaji  wa chakula.

Alisema kuwa kuna wakimbizi 10,000 kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanaohifadhiwa kwenye kambi ya wakimbizi Nyarugusu wilaya ya Kasulu ambao  wanafaidika na mpango huo na WFP inategemea  kufikia Desemba mwaka huu wakimbizi 70,000 wataingizwa  kwenye mpango huo,na  kiasi cha shilingi bilioni 1.4 zitakuwa zikitolewa kila mwezi kwa wakimbizi hao kuanzia Januari 2018.

Baadhi ya wanufaika wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamepongeza mabadiliko hayo,hasa kwa  misaada inayotolewa kwao kutoka chakula hadi fedha , hali  inayowawezesha kununua aina tofauti ya chakula wanachopenda na si  kupewa unga wa mahindi na njegere walizokuwa wanatumia tangu waingie kambini hapo mwaka 1996.

Nae Abiola Tabu Angeliq Raisi wa wakimbizi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu alisema kwa miaka mingi walitumia unga wa mahindi, njegere  na maharage ambayo wengi wao walitamani kuwa na chakula mbadala lakini haikuwezekana na hasa  wenye mahitaji maalum wakiwemo wagonjwa wa kisukari.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa makazi wa kambi hiyo kutoka Wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Alinda Batenga alisema kuwa mpango huo umesaidia wakimbizi kutopata muda wa kwenda nje ya kambi kwa ajili ya mahitaji ya chakula kwani kwa sasa mahitani yote ya vyakula yanapatikana kwenye soko la pamoja na itasaidia kuimrisha ulinzi na usalama.

0 comments: