UTURUKI IMEZIDISHA UJASUSI NCHINI UJERUMANI

Idara ya upelelezi ya Ujerimani BfV imeripoti kuongezeka kwa ujasusi wa Uturuki nchini Ujerumani, huku waziri wa mambo ya nje wa Uturuki akiitaka serikali mjini Berlin kuamua iwapo Ujerumani ni rafiki wa Uturuki au la.
Symbolbild NSU Affäre Verfassungsschutz Jahrestag Terrorismus Rechtsradikale (picture-alliance/dpa)
Idara ya uchunguzi wa ndani ya Ujerumani ya BfV, imesema mgawanyiko nchini Uturuki kuelekea kura ya maoni ya tarehe 16 Aprili kuhusu kuimarisha madaraka ya rais Recep Tayyip Erdogan imejitokeza nchini Ujerumani. BfV imesema katika taarifa kuwa inafautilia kwa karibu ongezeko kubwa katika juhudi za ujasusi wa Uturuki nchini Ujerumani, bila hata hivyo kutoa ufafanuzi zaidi.
Tayari uhusiano mgumu kati ya Ujerumani na Uturuki ulishuka zaidi mwezi huu, katika mgogoro kuhusiana na hatua ya polisi kufuta mikutano ya kisiasa kutafuta uungwaji mkono katika kura ya maoni ijao. Karibu Waturuki milioni 1.4 wanaoishi Ujerumani wana vigezo vya kupiga kura.
Akitumaini kutuliza mgororo huo siku ya Jumatano, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel alikutana na mwezi wake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu mjini Berlin. Wakati wanadiplomasia hao wawili walikubaliana juu ya umuhimu wa kudumisha uhusiano mzuri, Cavusoglu alisema Ujerumani laazima iamuwe sasa iwapo Uturuki ni rafiki au la.
Deutschland Treffen Gabriel und Cavusoglu (picture-alliance/dpa/K. Nietfeld) Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel (kulia) na mwezi wake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu wakiwa mjini Berlin, 08.03.2017.
Msitari mwekundu
Katika muktadha wa matamshi kutoka kwa Cavusoglu na rais Erdogan, Gabriel pia aliweka wazi kwamba katika kuendeleza uhusiano mzuri ipo misitari ambayo haipaswi kuvukwa. Na mmoja ya misitari hiyo ni kulinganishwa na Ujerumani ya enzi za manazi, alisema Gabriel.
"Tunataka kushirikiana vizuri na kwa amani na nchi hii, na kutafuta migogoro katika njia ya kidemokrasia, kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaetendewa kwa kukosewa heshima, na kwamba wanaweza kutegemea urafiki wa Wajerumani," alisema Gabriel.
Katika juhudi za kutafuta kuungwa mkono katika kura ya maoni ya mwezi ujao, Erdogan mwenyewe anatarajiwa pia kufanya mkutano nchini Ujerumani. Wakosoaji wameonya hata hivyo, kuwa mfumo unaopendekezwa wa rais ambao unataka kupanua madaraka ya Erdogan utaimarisha utawala wa mtu mmoja nchini Uturuki.
Ujasusi wa Uturuki nchini Ujerumani
Akisukumwa na wasiwasi kuhusu mgogoro kati ya Waturuki wa mrengo mkali wa kizalendo nchini Ujerumani na wafuasi wa chama cha Wakurdi cha PKK, rais wa BfV Hans-Georg Maassen alianzisha uchunguzi mwezi Januari katika uwezekano kwamba wahubiri wanaotumwa na Uturuki nchini Ujerumani wanafanya ujasusi.
Deutschland Verfassungsschutzpräsident Hans-Georg Maaßen (picture-alliance/dpa/M. Kappeler) Rais wa idara ya upelelezi wa ndani BfV Hans-Georg Maassen.
Maassen alisema ipo hatari kwamba malumbano hayo ya uwakala kati ya wafuasi wa PKK na wazalendo wa itikadi kali za mrengo wa kulia, yanaweza kuongezeka kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa hatari kwa pande zote.
Ingawa hakuzungumzia moja kwa moja suala la ujasusi wa Uturuki, Maassen aliwambia waandishi habari mwezi Januari kwamba Ujerumani haitovumia operesheni ua ujasusi za Uturuki ndani ya mipaka yake. Akirejea matamshi ya Maassen Jumatano, Gabriel alisema baada ya mkutano wake na Cavusoglu, kwamba malumbano ya ndani ya Uturuki hayapaswi kuletwa nchini Ujerumani.

0 comments: